Misaada; Mjane wa Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada; Mjane wa Daudi Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mp Kalix2, Oct 4, 2012.

 1. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi Utamaduni huu wa kuweka haki pembeni (Sheria)na kufarijiana kwa pesa hautatufikisha mbali na zaidi utatuletea yanayoendelea Somalia na kwingineko.Na shawishika kuwa bila kuwaona mbele ya Hakimu/mahakama kundi lote la wale askari waliopo sehemu ya tukio ikiwa pamoja na RPC wa Iringa iko siku! watoto wa Marehemu watatafuta namna mbadala ya kuona haki imetendeka dhidi ya Marehemu Baba yao.

  [FONT=&amp][FONT=&amp]Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo [/FONT]Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Ya Mjane Wa Mwangosi Na Wanawe Kupitia NSSF [/FONT]


  Napata shida sana kuamini haya mambo.Simshambulii Mhe.Zitto na wengineo wengi waliochangishana pesa kwa kumsaidia mjane wa Daudi Mwangosi.

  Lakini kwa imani yangu na ufahamu wangu mdogo nilionao, wasamaria wema hawa wangeweza kumtendea haki Marehemu pamoja na Familia yake na kuwapatia faraja Mjane na watoto wake kwa kuanza na jambo hili;

  KUSAIDIA KUFUNGUA KESI YA MAUAJI NA MADAI DHIDI YA JESHI LA POLISI NA SERIKALI.

  Kwamba wote walioshiriki na kusimamia kifo cha Mwangosi wanafikishwa mbele ya Mahakama na kesi yao kusikilizwa kwa uwazi kama wanavyofanya Mahakama za Kimataifa na hukumu kutolewa.

  Kwamba familia inahitaji kuhudumiwa au kulipwa na Serikali baada ya Jeshi la Polisi kuhusika na kifo cha Mzazi huyu ambaye ni tegemeo la familia kwa kila kitu.

  Misaada hii itamtoa Mjane wa Mwangosi toka utumwa wa Kilio cha ndani kwa ndani na kumletea faraja ya moyoni kwa kuona watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na kuridhika kwake kama mwenendo wa kesi umefuaka sheria.

  Lakini pia madai ya fidia italeta uhakika kwa familia kuendesha maisha kadri marehemu alivyokuwa akipigania maendeleo ya kuhudumia familia yake.

  Kwa upande mwingine naomba nimkumbushe Mhe.Zito anayedai anaweza kuwa amiri Jeshi Mkuu (Raisi)kwamba kama ni mimi hapa Mtihani mmoja mdogo unaelekea kuufeli.Kama Mbunge aliye na ndoto ya kuwa Raisi,nilitarajia ukipasa Sauti ndani na Nje ya Nchi kuwa RPC wa Iringa aliyekuwepo na kushiriki moja kwa moja na wale askari wote walioshiriki kwenye Kifo cha Daudi wanafikishwa mahakamani ,bila kusahau matukio mingine kama haya.

  Na kwamba Michango inayoendeshwa sehemu ya pesa hizi zilifaa zitumike kufungulia Kesi na kutafuta Mawakili watakaosaidia haki kutendeka /ionekane inatendeka.Shughuli hii wewe kama Msomi , Mbunge na mwenye ndoto ya kuwa Raisi na imani unaiweza na ni mtu muafaka kuisimamia kuliko hii ya NSSF kama utaamua kuifanya .

  Kwa Mjengwa blog na wanahabari wengineo nawashauri ili kumtendea haki Mwangosi na kama mlivyo andamana jangwani tafuteni namna ya kufungua Kesi ya kweli na ya haki dhidi ya kifo cha Daudi Mwangosi na hii itakuwa zawadi pekee mtakayoweza kumpatia marehemu.(Haki Mbele ya Sheria)

  R.I.P- D.Mwangosi
  Huu ni mtazamo wangu.
   
 2. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2013
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  Bado na amini kuliko kuchangishana kugenga minara na kuisaidia familia ya Marehemu.D.Mwangosi na hasa Watoto wake waliokuwa wakimtegemea kuona anawawezesha kuwa na Maisha Bora kuna haja ya kufungua Kesi Dhidi ya Polisi/Serikali na kudai Fidia kwa mtindo kama huu;

  JK AWAACHIA HURU POLISI WALIOMUUA JENERALI KOMBE ... [FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Ni mwaka moja umepita!

  Haya ni baadhi ya mambo unashindwa kuamini !
  Je mpaka leo ni kiasi gani imepatikana na imefanya nini?
  Kweli hii ni aibu kwa jamii inayolilia haki kutendeka!


   
 3. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Mchango mzuri makini. tatizo nnaloliona ni utayari na uthubutu wa kutekeleza hili suala.
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2013
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,096
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #5
  Oct 11, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mimi nimechangia leo unaniita mwizi au umekosa tusi l;eo?
   
Loading...