Misaada Imuezuiliwa, Sasa ni viongozi Kuzuiliwa

Misaada Imuezuiliwa, Sasa ni viongozi Kuzuiliwa

Drug-Czar

Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
16
Reaction score
39
Kutokana na aibu inayoendelea ya IPTL na Escrow, Nchi wahisani wameamua kuzuilia misaada kwa Tanzania. Na ingawa kuna ushahidiwa kutosha kwamba fedha za umma zimechotwa na mafisadi, viongozi waandamizi wamegoma kujiuzulu na chama chao CCM kikiwakingia kifua.

Ni swala la fedhea kusema kweli. Na aibu ya hapo mbeleni ni aibu mbaya sana, kwani viongozi wetu wamepoteza “Credibility” kuongoza nchi. Hakunakiongozi yeyote wa maana atakayeweza kufany kazi yoyote ya maana na Pinda , Muhongo, Maswi, Werema, Tibaijuka, Mramba, Chenge na wengine wengi ndani ya Serikali ya CCM. Hata Rais Kikwete mwenyewe atakuwa na wakati mgumu kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa asipowatema hawa Mafisadi (Majambazi Sugu)

Itakuwa ni aibu kubwa pale viongozi waandamizi kama Muhongo, Maswi, Werema na Tibaijuka watakapo wekewa zuilio kukanyaga ardhi ya nchi kama za Ulaya na Marekani. Hii haitakuwa ni aibu tu, bali itakuwa ni pigo kubwa kwa watanzania. Nadhani ni muda muhafaka kwa hawa watuhumiwa kuachia madaraka. Hawataweza kuyatekeleza majukumu yao kutokana na kashfa walizonazo.

Rais Kikwete chukua hatua kukinusuru CCM !
 
Back
Top Bottom