ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,050
- 61,376
Ikatokea nimefariki Mali zangu nitamwachia mke wangu kwa ajili ya maslahi ya familia yangu.sitathubutu kumwachia ndugu awe msimamizi.kumwachia ndugu cash au assets Ni sawa umemwachia fisi butcher ataipiga yote Kwanza anaweza kukuruka kuwa hujamwachia..kama huamini mtumie pesa ndugu yako wa kijijini akujengee nyumba halafu wasiliana Naye akikwambia imefikia labda kozi nne fanya ziara ya kushtukiza hakika utakuta hamna kitu ka forge cement kaweka ratio ndogo ili ajilipe posho.hivyo hivyo hata kwenye Mali zako mweke mke awe msimamizi hata Kama ataolewa Tena na mwanamme mwingine Basi atakumbuka kutunza hata watoto wenu.ni hayo tu kwa leo nimesema haya kwa sababu mtaani Kuna kesi flani ba mdogo kaachiwa asimamie Zaidi ya million kumi na marehemu Kaka yake kamsaliti Kaka kala pesa yote kabakiwa na milioni moja tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app