Mipango Mijii Dar Es Salaam na mikoani iwe updated

Mipango Mijii Dar Es Salaam na mikoani iwe updated

z12f

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
745
Reaction score
633
Mipango miji ya DSM (na sehemu nyingine za TZ) iwe updated ili kureflect population growth, population density, land use changes na sometimes abandonment of old government policies.

Unaweza kuta zamani sehemu fulani ilikua ijengwe bandari ndogo, hii ikawekwa kwenye mipango miji, sera hiyo haipo tena ila bara bara husika ni nene sana kwa sababu ya hiyo bandari ndogo. Au maviwanja makubwa sana wakati idadi ya watu imeongezeka.

Kule Kigamboni/Gezaulole mpango mji unaotumika ni wa 1992. Census kama tatu zimeshapita, mabadiliko makubwa yameshatokea. Nahisi na maeneo mengine ya DSM kama Mbezi juu, Goba, Bunju etc yatakua hivyo hivyo.

Mtu moja moja kufanya amendments za ramani yake huwa ni time consuming na expensive, halafu huwa ni limited in scope kwasababu amendments kama hizi haziwezi kubadilisha unene wa barabara e.g. kufanya barabara yenye unene wa mita 100 kuwa na unene wa mita 50.

Halafu nadhani maeneo ya kuzikia/makaburi yameanza kuwa machache (DSM na sehemu nyingine).

Madampo ya uchafu naona kama yamezidiwa kidogo. Halafu kuwe na madampo ya recyclable waste and non-recyclable waste. Na madampo ya toxic waste kama heavy metals (mercury, lead etc). Hii itasaidia kutunza mazingira. Utunzaji mzuri wa mazingira ni muhimu sana hususan maviwanda yakianza kuongezeka na watu wakianza kutupa taka taka nyingi za majumbani.

Ku update mipango miji ni very expensive, lakini ni vizuri kuanza kidogo kidogo.

Serikali itarget urbanisation rate ya 50%. Yaani nusu ya watu wanaishi mijini na nusu wanaishi vijijini.

Mji wa Dodoma uwe na watu around 3 million. Kuwe na maeneo ya kutosha ya biashara huko Dodoma. Maji yavutwe kutoka Iringa au Morogoro. Mikoa yote iunganishwe na barabara za moja kwa moja kutoka Dodoma. Watu wapewe viwanja kwenye ruti za kwenda mikoa yao ya asili. Ili kama zikitokea vurugu huko mbeleni iwe rahisi kuzikwepa.


Mji wa Dar uwe na stendi za mabasi za mikoani tatu. N makariakoo matatu. Moja kwa ruti ya kusini (Kilwa road), ingine ruti ya morogoro road na ingine ruti ya new bagamoyo road.

Mji wa Arusha uwe na viti viwili vya ubunge.
 
Bila kusahau sewage systems. Kama budget itakavyo ruhusu.
 
Hivi Dar wana kitengo cha mipango miji, wanafanya kazi gani hao watu?
 
Kwa sasa kinachofanyika ni Urasimishaji makazi holela kwa kuyapima maeneo ambayo watu wameshajenga.Hii Inaitwa regularization of informal settlements au squatter upgrading,huu ni upimaji shirikishi. Nawaasa watu wote ambao upimaji wa aina hii unafanyika washiriki kikamilifu maana gharama zake ni ndogo na watanufaika kwa kupata hati na pia serikali itapata kodi(hili ni lengo kuu).Hii inafanyika maeneo kama Makongo juu, Kimara Matangini,Kilungure,Goba n.k
 
Back
Top Bottom