oruguyo
Senior Member
- Jul 28, 2012
- 132
- 37
Ni kweli tunatakiwa kulaani vitendo vyote vinavyosababisha kumwagika kwa damu za watu wasio na Hatia lakini tukumbuke Mto Ruvu watu wameokotwa wameuwawa tukaambiwa ni wahamiaji Haramu. Ni kweli?
Saanane kapotea, wengine juzi wakasema amejiteka na anatafuta umaarufu. Bashe, Msukuma na Malima wametekwa, wamelalamika hawasikilizwi. Nape Bastola imetolewa mchana peupe, hakuna hatua iliyochukuliwa kwa huyo gaidi aliyetoa bastola.
Roma na wenzake wametekwa, tukaambiwa ni tukio kama matukio mengine ya kiuhalifu. Clouds Media wamevamiwa tukaambiwa ni vikosi maalum wakishirikiana na Bashite, Wawakilishi wakapaza sauti kuwaeleza wanaodhani nchi ni yao peke yao wakasema hakuna shida hayo ni maneno tu.
Sasa viongozi yawapasa wajitathimini. Raisi na familia yake wanatembea chini ya ulinzi, mawaziri vivyo hivyo, Wakuu wa Mikoa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi Mnalindwa. Kumbukeni hao ndugu zetu wanaouawa ndo tuliokuwa tunawategemea katika koo na familia zetu. Maamuzi yenu na ukimya wenu unatusababishia majonzi mioyoni mwetu.
Hakika nimewahi kuandika hapahapa kwenye forum hii kama mngeweka kura za siri kwa watanzania na Jeshi la polisi wawaeleze yaliyoko mioyoni mwao hakika mngegundua hakuna aliye tayari kuitetea nchi hii. Shida ndo zimetuweka ktk kazi za Serikali. Isitoshe ninyi mnaodhani mmemilikishwa madaraka na Mungu aliye juu mmekuwa ni sehemu na chachu ya kuchukiwa kwa Polisi huku Mitaani.