Mind You, Uongo Sio Mzuri

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,885
Wanaume wenyewe tunafahamu, kwamba ili ufanikiwe kumnyakua malkia mmoja na kumuweka katika ufualme wako ni lazima uwe na ulimi wenye chembechembe fulani za uongo hivi ujue kupangilia maneno, kuigiza na kuumba matukio na kuyapa uhai kana kwamba yalishawahi kutokea.


Zaidi mwanaume unatakiwa kuwa kama kinyonga, unabadilika kulingana na mazingira. Ukishajua mrembo unayemfuatilia anapenda kusikia unafanya kazi kwenye ofisi yenye kiti cha kuzunguka ‘full’ kiyoyozi, una ka-gari ka kumpeleka ‘out’ na pesa za kutambia mjini basi vaa uhusika haraka.

Anza kwa kununua mashati mawili matatu vile wafanyakazi wa benki wanapenda kuvaa, changanya na tai fulani hivi, chini suruali ya kadeti iliyokwenda shule na moka kali ya ngozi kutoka Italia na kama huwezi kununua yote haya, hata kuazima inakuwa sawa tu, ilimradi lengo lifanikiwe.

Ukirudi kwenye gari, hata kama katika ukoo wenu wote hakuna anayemiliki hiyo kitu, wewe kachongeshe hata funguo uwe unaing’iniza kwenye suruali kila mkikutana, halafu sasa tumia ule ujuzi wako kuumba matukio, jifanye una gari ila lilipata ajali juzi juzi, tena mzinga wa maana kwa hiyo lipo gereji njia hii ni kwa ajili ya kukusaidia kupunguza gharama za kuingia ‘sheli’ kwa sababu hutohiaji kuazima gari.

Kitu cha muhimu na cha mwisho ni uzungumzaji, hakikisha kila neno linalotoka kinywani mwako linafafana na jinsi ulivyojitambulisha kwake. Kama ulijatumbulisha kuwa wewe ni ‘Finance Manager’ wa Fandago Company, hakikisha unazungumza kama mmoja wao ongea polepole na usisahau kuchanganya na kizungu kidogo ila kumbuka matokeo yoyote utakayoyapata ni wewe mwenyewe utakayewajibika.
Hata hivyo, kuna siri ambayo ni wachache wanaifahamu.

Ni kwamba ndoa nyingi za mijini hasa Tanzania kama sio duniani kote zimeundwa kwa uongo uongo tu. Mwanamke anaanzisha uongo wa kwamba haujui ugali na mwanaume anauendeleza uongo wa kwamba ana pesa ya kumnunulia mapochopocho kwa kipindi chote watakachokuwa pamoja.

Mwisho wanashtukia wameshakuwa mke na mume na wana watoto pia. Mwanaume anagundua kuwa kumbe mke wake anafahamu aina zote za ugali , kuanzia wa sembe hadi wa mtama na mwanamke anagundua kuwa kumbe mume ni pangu pakavu, zile zilikuwa mbwembwe tu.


Tabia hii ya uongo ndiyo inayompasua kichwa jamaa yangu Kamugisha kiasi kwamba sasa hivi amekuwa kama mwendawazimu hivi. Msongo wa Mawazo wa kujitakia unamuandama, uongo alioufanya miaka 10 nyuma umeanza kumtesa sasa.

Kamugisha wakati anamchumbia mke wake si alimdanganya amesoma mpaka chuo kikuu, eti akahatimu na ndani ana gamba lake la shahada ya ugavi na ununuzi.

Lakini kumbe hamna kitu, aliishia kidato cha nne, akaungaunga anavyojua mwenyewe matokeo yake akapata cheti kweli na akalamba ajira serikalini.

Sasa leo hii kaona jina lake kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki aliyopewa mkulu. Akili zimemruka hatari, anafikiria jinsi gani ataendelea kuupa uhai ule uongo aliomdanganya mke wake mika 10 iliyopita, atamwambiaje ili heshima yake isishuke.


Hata hivyo, juzi kuna mtu alimshauri akamwambia akiirudi nyumbani aongeze uongo mwingine, amwambie mke wake kuwa kazini wametangaziwa kwamba serikali haina pesa, inataka kupunguza watu, kwahiyo wanaotaka kujipunguza wenyewe waanze. Kwa hiyo aseme yeye ameona bora aachane na hiyo kazi kwa sababu wanapoelekea hata mishahara wataanza kulipwa tarehe 40.


Ni uongo mzuri ila inategemea ameoa mwanamke wa aina gani; kama ni mke wa Instagram atafanikiwa, wanawake wa hivi hawanaga muda wa kufuatilia habari za Magufuli na Serikali yake, wenyewe ni Shilole na Nuh Mziwanda tu.
 
Heshima Mkuu!

Las mentiras son necesarias cuando la verded es muy dificit de creer.Huo ni msemo wanao wafaransa, Wanamaanisha hivi "Lies are necessary when the truth is very hard to believe".

Ni kauli ngumu kidogo, ila sometimes inabidi iwe applicable panapostahili.Nb;Si mara zote lakini.

Mungu atupe nguvu tulio na vyeti feki.
 
Wewe kama sio uvccm basi utakuwa ni MTANGAZAJI wa TBC aitwaye Gabriel Zakaria, maana huko ndiyo kuna vyuo vya uongo
 
Hahah nimeipenda "mshahara tutalipwa tarehe 40" kweli ila uwongo si mzuri.
 
Back
Top Bottom