Mwenyekiti Kijiji cha Kwa Zoka na wengine watatu mbaroni kwa kusambaza taarifa za uongo za watoto kutekwa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,197
4,475
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kurekodi na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gari aina ya Toyota Noah inayotumika kuwateka watoto katika maeneo mbalimbali.

Kuhusu utekaji huo soma > Utekaji wa watoto: Gari yadaiwa kukamatwa ikiwa na watoto wawili waliotekwa

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kwamba watoto wawili wanaosoma Shule ya Msingi Vigwaza wametekwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema watu wao ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwa Zoka, Shomari Zinga, (64) Aishi Ally (32), Alphonce Temba (34) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Vigwaza na Paul Mwanilezi.

“Taarifa hizi zilienea kwa haraka hadi Shule ya Msingi Mtongani iliyopo Mlandizi wilayani Kibaha na kuleta taharuki kwa wazazi, walimu na Watoto wa shule hiyo ambapo mzazi Zaituni Shabani alieleza kuwa mtoto wake Isimaiya Zuberi (6) ni miongoni mwa watoto waliotekwa,” ameeleza.

 
Wamejuaje kuwa ni za uongo badala ya kufanyia kazi wao watoa taarifa wanawakamata pana kitu hapa sio bure inakuaje Polisi ya Puerto Rico inawalinda Watekaji..
 
Tumwamini Mwenyekiti au Polisi?

Labda iundwe tume huru itakayosaidia ukweli kufahamika.

Tume iwe na jukumu la kubaini mwongozo kati ya Polisi na Mwenyekiti wa kijij.
 
Sitasahau nilienda kulipoti mtu kaumizwa kadondoka baada ya kufanya upelelezi naanza kuwekwa mimi ndani.
Tokea siku hiyo serikali na polisi walishasema drama
 
Back
Top Bottom