Kwa uwazi kabisa mimi ninaafiki utawala wa Mhe. Magufuli kwa asilimia mia moja na nchi hii inataka kiongozi DIKTETA angalau kwa miaka mitatu au minne ijayo kutokana na sababu zifuatazo:-
- Kuna watu wachache nchi hii wanayomiliki ukwasi unaotisha kwa mgongo wa Watanzania. Huku wananchi wengi wakiwa kwenye lindi la umaskini.
- Nchi hii utakuta mtu anatembelea gari ya shillingi bilioni moja kwa mgongo wa Watanzania bila kuulizwa.
- Nchi hii watu wachache wana mahekalu ya ajabu kwa mgongo wa Watanzania.
- Nchi hii watu wachache ndiyo wana sauti na wanaweza kufanya lolote bila kuulizwa na yeyote.
- Nchi hii ni watu wachache wanaweza kufunga mikataba yenye harufu ya kifisadi na hakuna wakuwauliza huku wananchi wanakosa huduma za kijamii kama shule,zahanati nk.
- Nchi hii ni watu wachache wanaua tembo na hakuna wakuwauliza.
- Nchi hii wachache wanaweza kuwanunua vingozi wa Serikali kwa manufaa yao.