Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,311
- 152,112
Kwa huu unyama tunaoushudia mimi ndio maana siku zote huwa nashindwa ku-comment RIP watu fulani fulani wanapotangulia mbele za haki na kwakweli hizi comments binafsi huwa zina ni kera sana.
Ingawa kila siku tuko makanisani na misikitini tukijidai tunaenda kumuomba Mungu lakini sisi binadamu ni viumbe wenye roho mbaya na makatili kuliko hata wanyama.
Binadamu wa leo tumepoteza utu tumekuwa kama mashetani na tuna roho mbaya kuliko hata Ibilisi.
Kwa mfano,angalia comments za watu wanaotetea huu unyama kisa tu wana mahusiano au wa na namna wanavyofaidika na uwepo wa watu wanaohusika na huu unyama.Huu ni ubinafsi mbaya sana wa kiwango cha ushetani na watu hawa baadhi yao kila Ijumaa au Jumapili utawaona wakielekea kwenye nyumba za Ibada eti wanakwenda kusali.
Wanaoyatenda haya wanajulikana na wala hayakuanza leo bali huu ni utamaduni wao wa muda mrefu na wanachofanya ni kuuendeleza tu kwahiyo hapa hakuna jipya.
Cha ajabu na kusikitisha,watu wa aina hii na wale wote wanaotetea huu unyama kesho na keshokutwa Mungu akiwachukua utaona watu wako busy ku-comment RIP!!!.
Binafsi ningekuwa mmiliki wa mitandao kama hii,ningezuia kabisa neno hili la "RIP" kuandikwa katika mtandao wangu maana sisi wanadamu ni wanafiki sana na tunathamini binadamu kulingana na nafsi zao katika jamii bila kujali ni namna gani waliishi katika huu ulimwengu.
Hakuna mwenye haki ya kuhukumu mwingine lakini vitabu vitakatifu vinatueleza wazi ukishakufa kama hukutubu madhambi yako hakuna kitakachobadilika hivyo neno hili la RIO ni unafiki mtu na kwakweli linakera pale linapotumika kwa watu waliotendea binadamu wenzao unyama kwa maslahi yao.
Ni bora mnyama asie na dini kuliko baadhi ya sisi binadamu tunaojazana katika nyumba za ibada tukijidai kumuabudu Mungu wakati ni wanafiki wakubwa.