Mimi napenda mfumo dume' wewe je?

JJ10

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
282
Reaction score
133
Habarini wanaMMU!

Ivi ulishawahi kutafakari na kujiuliza ni mfumo gani unaotumia kuendesha maisha yako ndani ya ndoa?

Kama hujui basi huu ni mda mwafaka wakuliangalia hili' huenda ikaboresha maisha yako ya ndoa.

Maisha ndani ya ndoa yana mifumo mitatu. Kama ifuatavyo;

A) Mfumo Dume - mfumo huu ulitumiwa sana enzi za mababu zetu. Yaani baba ndo kichwa cha familia, baba ndo mwamuzi mkuu na ndo msemaji wamwisho wakila jambo linalohusu familia. Kwenye mfumo huu ndoa zilidum sana, maadili yalizingatiwa na kulikuwa na nidhamu ya hali ya juu katika familia hadi jamii kiujumla. Paka hivi sasa mfumo huu inaendeshwa na familia chache sana.

B) Mfumo wa Usawa - huu mfumo umeanza miaka ya hivi karibuni na paka sasa unazidi kushika kasi ya ajabu. Kwenye mfumo huu mwanaume hafanyi jambo bila kumshirikisha mkewe' na mwanamke vivyo hivyo! Hii ni matokeo ya haki sawa inayohubiriwa na mataifa ya magharibi na kupokewa na wanawake wakiafrika bila kuangalia athali za hiyo katika maisha ya baadae. kwenye mfumo huu ndoa zinalegalega sana na nindoa chache zina amani. Ingawa wanawake wanaupenda sana huu mfumo.

C) Mfumo jike - huu mfumo maisha yanaendeshwa na matakwa ya mwanamke ndani ya ndoa! Atakalotaka mwanamke ndilo litakalotekelezwa' baba ni muitikiaji na mtekelezaji wa maamuzi ya mama! Ndoa za namna hii zipo na zinaendelea kuwepo ingawa nivigumu sana kuzitambua kwa nje' paka uingie ndani sana au utokee mtafaruku ndo afunguke.

Vile utakavyoishi na mtu wako toka mkiwa wapenzi au mwanzoni mwa ndoa yenu ndivyo mtakavyoishi maisha yenu yote! Ni vigumu sana kubadilisha mfumo ndani ya ndoa' na ndoa nyingi zinavunjika pale mtu anapotaka kufanya mabadliko ya haraka baada yakugundua kwamba mfumo alioanzisha sio sahihi.

Ushauri; Ukiwa kwenye upenzi, uchumba au ndoa changa DON'T PRETEND' uwe wewe mtu akujue vizuri mapungufu na mazuri yako! Apime na anavofanya maamuzi asije yajutia baadae. Ukipretend alafu baadae unaanza kuonyesha tabia zako halisi kama surprise lazima ndoa iyumbe kama si kuvunjika kabisa. Hii itawafaa na kuwasaidia wenye mahusiano yenye tija na wenye malengo yakuishi maisha yafuraha ndani ya ndoa zao.

Umechagua mfumo upi kwenye ndoa yako?
Wewe ambaye bado ungependa kutumia mfumo upi?

Karibuni kwa mchango, kukosoa, au lolote lile unalojiskia kulisema.
 
^^
Mada nzuri sana! Na imefika siku husika.
Najaribu kutazama harakati za wanawake, naziona ni juhudi za wao kuwa wanaume!
^^
 
^^
Mada nzuri sana! Na imefika siku husika.
Najaribu kutazama harakati za wanawake, naziona ni juhudi za wao kuwa wanaume!
^^

Sawa kabisa mkuu!! Wanatafuta uanaume kwakasi ya ajabu' na wanasahau kuwa sio kwamba tu wanapotea bali wanapingana na maandiko matakatifu.
 
Sawa kabisa mkuu!! Wanatafuta uanaume kwakasi ya ajabu' na wanasahau kuwa sio kwamba tu wanapotea bali wanapingana na maandiko matakatifu.

^^
Siku hizi, maandiko matakatifu ni kama yapo yasomwe sio kutendwa
^^
 
Kwangu mimi mfumo wa usawa ndiyo mzuri zaidi na haiondoi maana ya kwamba Mwanaume ndiyo kichwa cha nyumba iko hivyo na itaendelea kuwa hivyo,upo wajibu wa mwanaume kama mwanaume as kichwa cha familia,na upo wajibu wa mama as mama kama msaidizi wa baba,kikubwa ni kupendana,kuheshimiana,kusikilizana na kila mmoja kujua wajibu wake katika ndoa.
Msimamo wangu ni kwamba katika ndoa wanandoa wote ni mwili mmoja unaanzaje kumtenda mabaya / kumkandamiza mwenzio wakati ni sehemu ya mwili wako? ina maana kwamba kama aidha baba au mama ataendesha ndoa yake vibaya ni kwamba anaharibu maisha yake mwenyewe tena anajikandamiza mwenyewe,haihitaji kujua ya kwamba huu ni mfumo dume,jike au usawa ambao utaleta amani.
 
Sawa kabisa mkuu!! Wanatafuta uanaume kwakasi ya ajabu' na wanasahau kuwa sio kwamba tu wanapotea bali wanapingana na maandiko matakatifu.

kwa mwanamke mwenye kujitambua wala haihitaji kuutafuta uanaume,tatizo lililopo tafsiri ya usawa ndiyo inachukuliwa vibaya.
 
maandiko matakatifu yanasemaje ??

wanawake wamejisahau kabisaaaa!!!
 
Mfumo dume is the best! Lakini it has to be EARNED! Kuwa kiongozi katika ndoa si jambo rahisi kama mwanaume hufanyi efforts za kuwa pale juu!
Uwe na busara, hekima, maarifa ya kutosha kuliko wale unaowaongoza! Uwe mfano mzuri kwa tabia njema, Uweze ku provide kwa familia yako na uwe ndiyo mtatuzi Mkuu wa matatizo yote na si kuyakimbia! Ubebe majukumu ya kulea, kutunza na kupelekea ustawi wa familia yako! Hapo utaheshimika na mwanamke na familia nzima kwa ujumla! Automatic na mke ambaye ni msaidizi wako ata assume nafasi yake bila kinyongo wala manung'uniko!
 
Hii phenomenon is just state of mind ambayo kaileta mwanadamu kutokana na maono na matakwa yake but in real sense hakuna kitu kama hicho
 
Mfumo dume ndio kila kitu. Haya mengine yooote hayakuwa mpango wa mungu
 

Simu yangu haina like ningekumwagia za kutosha
 
sijaisoma habari yenyewe,nimeona ni ndefu ila kwa kuona tu mfumo dume bila kujali kilicho ndani nakuunga mkono asilimia mia!naupenda sana huu mfumo na umeniwezesha kuwa na amani katika familia yangu!
 
Hii phenomenon is just state of mind ambayo kaileta mwanadamu kutokana na maono na matakwa yake but in real sense hakuna kitu kama hicho

Wewe umeongea sawa kabisa, mfumo dume,jike na sijui usawa yote haya kayaleta mwanadamu, katika maana halisi ya ndoa hakuna kitu kama hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…