Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,277
- 33,879
Wali plain siyo!?True pia palikuwa ni makutano point ya wajanja wengi wa mjini,
Hata sisi wanafunzi wa CBE 2010 ilikuwa ndo kijiwe cha kuvizia dinner ya bei rahisi punguzo bei kuanzia saa nne usiku
Mixer chochote walikuwa wanapunguza bei sahani kwa elf 2 badala ya elf 4 ikifika saa nne usiku sijui kama Bado wanautaratibu huo this daysWali plain siyo!?
Gen z wao wanakutana kidimbwi kitambaaa cheupe wanaongea mipango yaoGen Z watakuelewa kweli ha hizi story za kwenye kijiwe cha kahawa ?
Kiukweli hii bomoa bomoa imekuwa tatizo kubwa. Miaka kadhaa ijayo hakutakuwepo na kumbukumbu yoyote ya Dsm.Tuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.
Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.
Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
Oh nami umenikumbusha,mimi sheikh said nilikujulia hapo salamander kwa akina hashim sagaf,nilikuwa nakuja hapo na kaka yangu wakati huo nikisoma nje ya nchi,nikawa a bit rafiki kwako kutokana na uwezo wako wako wa kuchambua mambo,pia nikamfahamu jamaa mmoja akiitwa tamim,na kijana mmoja kama msomali hivi akiitwa mohamed akiaandikia magazeti.Kaka yangu akanipeleka hapo chef pride chagga street,aisee kulikuwa na kila aina ya chakula na ndipo nikakutana na watu wengi sana maarufu,na kabla sijasahau pale salamander nilikutana na jakaya na tukawa marafiki sana nadhani wakati huo alikuwa waziri wa madini.MIMI NA CHEF PRIDE
Historia yetu sasa nadhani ina kiasi cha miaka 30 na zaidi.
Mgahawa ulikuwa Mosque Street, Zahir Hotel.
Katika miaka ya 1980/90 ndipo kilipokuwa kijiwe chetu cha mazungumzo, kula na kunywa.
Mwendeshaji wa mgahawa kijana mwenzetu Salim Mahsen.
Vyama vingi vilipoanza 1992 mgahawa ukawa uwanja wa siasa wanachama na wapenzi wa vyama vyote huwapungui hapo.
Mijadala moto moto ikiunguruma.
Unachagua mwenyewe ukae meza ipi.
NCCR Mageuzi na Augustino Mrema ilikuwa imepamba moto, NRA kisha CUF ya Maalim Seif na Kaka Mkubwa CCM.
Salim anatununulia magazeti yote wa nyakati zile anatuwekea mezani - Shaba, Rai, Bahari, Uhuru na haya magazeti yalikuwa yana mkondo wake katika siasa changa za vyama vingi.
Ukifika Zahir asubuhi kunywa chai unapata taarifa zote katika ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Salim akiijua saikolojia ya sisi wateja wake.
Wakati mwingine akitutania anasema, "Nimekuwekeeni hizi meza ziwe mbali ili msiibiane sera."
Siku alipotuambia kuwa anairudisha hoteli kwa mwenyewe ilikuwa msiba.
Wateja wote tulitawanyika.
Hatukuwa na mahali pa kukutana.
Mgahawa ulikuwapo lakini haikuwa kama alipokuwa Salim.
Uwanja hakika ulikuwapo lakini magoli yameng'olewa.
Salim akafungua Chef Pride, Chagga Street.
Haba jana.
Tukapata uhai mpya.
Kisha akafungua Chef Pride nyingine Lumumba Avenue karibu na CCM.
Chef Pride hakika leo ni sehemu ya historia ya Dar-es-Salaam.
Hapati mtu mgeni sharti atampeleka Chef.
Chai ya asubuhi haipiti ila inywewe Chef.
Halikadhalika chakula cha mchana na usiku ukiwa na mgeni.
Nimeweka hapo chini picha ya Salim na Dr. Harith Ghassany nilipomfikisha Chef miaka michache ya nyuma nikamjulisha kwa Salim.
Chef ni mahali utamuona kila mtu.
Ni suala la subra na muda.
View attachment 3320767
Kulia Dr. Harith Ghassany na Salim Mahsen
View attachment 3320770
Carl Lewis alikuwa mwamba alitingisha sana enzi zakeTuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.
Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.
Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
Kule Arusha meeting point ya waalimu wakipokea mishahara ni Jogoo house karibu na stendi kuu. Waalimu wakuu na watendaji wa kata hukutana Stanley bar. Wanakuwa na mihuri kabisa... kama kuna ishu anakugongea muhuri chap.Moja ya mgahawa kongwe
Meeting point za watu wa mjini hizo
Ova
Salamander nayo ilishapoteaTuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.
Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.
Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
HahahKule Arusha meeting point ya waalimu wakipokea mishahara ni Jogoo house karibu na stendi kuu. Waalimu wakuu na watendaji wa kata hukutana Stanley bar. Wanakuwa na mihuri kabisa... kama kuna ishu anakugongea muhuri chap.