Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
ZANZIBAR haiwezi kujengwa bila ya kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi na ushiriki wa viongozi wa Chama Cha CUF katika shughuli za miradi ya maendeleo ni mafanikio ya umoja huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume aliyasema hayo katika ufunguzi wa skuli mpya ya Mjini Kiuyu Shehia ya Kiuyu Minungwini katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo viongozi mbalimbali wa chama na serikali walihudhuria wakiwemo viongozi wa chama cha CUF.
Katika hotuba yake aliyoitoa katika sherehe hiyo, Rais Karume alisema kuwa yeye mwenye binafsi amefarajika kuona ushiriki wa viongozi wa Chama Cha CUF katika sherehe hizo na kusisitiza kuwa huo ndio umoja na mshikamano ambao unajenga amani, utulivu na upendo na kuahidi kuusimamia.
Alisema kuwa Wazanzibari wote ni wamoja hivyo kuna kila sababu ya kuishi kwa upendo na maelewano hatua ambayo itaipeleka mbali Zanzbar katika kuimarisha uchumi wake na miradi yake ya maendeleo sanjari na uimarishaji wa amani na utulivu.
Sisi Wazanzibari wote ni wamoja na wala wasitokee watu wakatudanganya tukajigawa na ili uwe Mzanzibari ni lazima utokee Unguja ama Pemba na hata ingekuwa si wamoja kwani ingekuwa vibaya kuungana, mbona leo Ulaya wameungana na kuunda (EU) ambapo ni nchi nyingi na watu wake ni wengi na wanaongea lugha tofauti,alisisitiza Rais Karume...
Source: Zanzibar yetu web blog