Kayenga jr
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 443
- 349
Kosa kubwa wanalolifanya watu wenye shida ya uzazi ni kuruhusu presha ya mtoto itawale maisha yao, presha ya marafiki, ndugu na majirani haipaswi kuwatawala.
Japo kweli ni stress lakini mnapaswa muweze kuicontain,
Kimsingi hapo pana mambo mawili,
Kwanza inaonekana bibie alikuwa na shida ya mimba kutoka na mimba za chini ya miezi 2 kama nimekuelewa vizuri, hii sio shida sana kwa mimba kutoka miezi mitatu ya kwanza, asilimia kubwa ya kisababishi ni chromosomal abnormalities, mwili unakuwa umeona kuna shida juu ya kiumbe kilichopo na kuamua mimba itoke ili isilete kiumbe cha ajabu, (so mostly is a protective mechanism).
Lakini pia kuna vitu vingine kama maambukizi kama hayo ya Rubella, syphiliis, toxoplasmosis, cytomegalovirus, na Hepatitis.
Pia vitu kama antibodies (antiphospholipids antibodies) huweza kuwa sababu ya mimba hizi kutoka.
Kama alikuwa na Rubella probably ilikuwa inachangia kwenye shida hiyo, ila kwakuwa imetibiwa ni vyema kupima tena na kuhakikisha kuwa hana tena hayo maambukizi,
Chapili inaonekana ana shida nyingine ya mirija ambayo hii husababishwa na maambukizi kwenye njia za uzazi (Pelvic inflammatory disease) hii huweza kupelekea mirija kuziba kabisa na kusababisha asiweze kushika mimba (tofauti na mimba kushika na kutoka).
Kwa maelezo yako inaonekana hapo awali hii haikuwa shida maana aliweza kushika mimba, lakini pia kuziba mrija mmoja bado unabaki mnoja na huo uliobaki unaweza kusafirisha ovum na kutunga mimba.
Swali ni je Maambukizi haya yaliyosababisha mrija kuziba yalitibiwa!??
Kama hayakutibiwa yawezekana yaliendelea na kusababisha mrija wa pili pia kuziba, (NOTE:Maambukizi haya ni tofauti na yale ya Rubella na huwa hayanaga dalili nyingi za kujionyesha au huchelewa kujionyesha)
Na hayo maumivu wakati wa siku zake (dysmenorhoea) moja ya visababishi ni haya maambukizi yani PID,
WHAT TO DO!
Mrudi hospital bila kuchoka maana shida yenu haitibiwi kwa mkupuo, inatibiwa kwa process, inahitajika mfanye Ultrasound tena kuona viashiria vya PID na vikiwepo atibiwe vizuri pia mtapaswa kurudia HSG kuona hali ya mirija, kwakuwa hormone zilikuwa sawa na assuming hamjatumia dawa zozote za ki-hormone hii kwasasa sio ishu,
Baada ya hayo mtapaswa kupata muda wakujaribu kutafuta mtoto haswahaswa kwa kuzingatia zile siku nzuri kwenu kwenye kalenda (ni jambo zuri kuwa siku zake hazibadiliki hovyo)
Majibu ya Vipimo pamoja na matibabu ya vitakavyobainika yatadetermine nini kifuate.
Nakutakia kila laheri
Asante kakaKama Mungu alifanya kwa watu wa zamani ,akafanya kwa vzazi vya sasa na leo pia yupo tayar kufanya kwako kama utamtegemea.Wala usijiingize katk imani potofu we piga got ongea na Mungu wako.Mungu anasubir upeleke hoja zako mbele zake naye atafanya
Pamoja ila mi dada.Asante kaka
Poa kumradhi jina hilo sijalielewa vizuriPamoja ila mi dada.
Wee acha tu yaanInaumiza sana...pole sana bro Mungu akujaalie hitaji la moyo wako,pia akupe wepesi wa kusubiri.
Poa pamojaMiaka minne sio mingi hadi ukate tamaa, kinacho kucost hadi sasa ni pressure uliyonao inayotoka kwa marafiki, ndugu pamoja na majirani wanaokuzunguka. Tuliza akili yako mkuu weka imani yako kwa Mwenyezi Mungu halafu anza kutafuta solution ukiwa na amani moyoni mwako, usipanic hilo ni jaribu lako nawe huna budi kulishinda
Ila kwa7bu ulishapima ukaonekana upo safi na doc kasema shemeji anaweza akafanikiwa kupata ujauzito nadhani ni kumwachia tu Mungu atatenda kwa wakati wake,wengine wanakaaga miaka kumi muhim nikuheshimiana na kufarijiana ndani ya nyumba,pia utulivu uwepo mengine yatajiset yenyewe,Abraham alipata mtoto akiwa na 80yrs kaka Mungu ataleta neema hakukupa mke then asikupe mtoto.Wee acha tu yaan
Nakushukuru sana kwa ushauri kaka mungu akubarikia ningeomba kama utapata mawasiano ya huyo bibi sio mbaya nikajaribu njia zote za kienyeji na hospitalPole sana, kwanza ondoa hofu, I miaka 4 sio mingi, hasa kama utaishi maisha yako wewe na mkeo bila kuruhusu ndugu/marafiki kuwaingilia.
Nime pitia katika hali kama yako, na japo ina tofauti kidogo, namshukuru Mwenyezi Mungu sikuwapa ndugu/marafiki nafasi la sivyo ningekuwa na hali mbaya.
Mkewangu kwanza alichopewa kushika ujauzito, mpaka mwaka wa kwanza wa ndoa ukaisha. Ndani ya miezi 3 tu ndugu/marafiki washaanza kuulizia kama tayari.
Kuja kushika mimba, zinatoka mara 2, mara ya 3 ikatungwa nje ya kizazi na tukachelewa kugundua mpaka ikapatikana na akaanza kuboresha ndani, akifanyiwa upasuaji.
Tuli hangaika sehemu mbalimbali mpaka kwa Dr Mwaka na kwa maspecialist ila kikubwa sote tulikuwa hatuna hofu sana wala shauku kwasababu tulikuwa tuna imani kuwa mtoto anatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Baada ya mahangaiko Mwenyezi Mungu akujaalia kushika tena na sasa unaelekea mwezi wa tatu Alhamdulilahi hakuna tatizo lolote kubwa mpaka sasa.
Kubwa, kwanza tambua mtoto ni baraka kutoka kwa Allah subhanahu wataala, hivyo msiwape presha sana tambueni wakati ukifika kama karanga mpate mtoto mtapata tu.
Pili kuwa karibu sana na mkeo na hata kama una hamu sana na mtoto jitahidi usi muonyeshe na untie moyo, tambua kuwa wana wake ndio wanao umia zaidi katika hali kama hiyo hivyo wewe ndio msaada wake mkubwa.
Kubwa na la mwisho usijidanganye kutoka nje ya ndoa kwenda kutafuta mtoto, unaharibu kabisa dira ya maisha yenu, zinaa ni deni na malipo yake yana tisha kabisa
Endelea kukazana na kutafuta tiba na kumtegemea Mwenyezi Mungu, yeye ndie ajuaye ghaibu.
Kuna bibi mmoja chanika mkewangu aliwahi kutibiwa huko, ana dawa nzuri na za gharama nafuu, kama hauja wahi kujaribu huko nta kutafutia mawasiliano yake.