Kayenga jr
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 443
- 348
Ndugu wana JF doctor,
Nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.
Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.
NikampelakaRecency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushika tu imekuwa tatizo.
Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.
Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.

Kosa kubwa wanalolifanya watu wenye shida ya uzazi ni kuruhusu presha ya mtoto itawale maisha yao, presha ya marafiki, ndugu na majirani haipaswi kuwatawala.
Japo kweli ni stress lakini mnapaswa muweze kuicontain,
Kimsingi hapo pana mambo mawili,
Kwanza inaonekana bibie alikuwa na shida ya mimba kutoka na mimba za chini ya miezi 2 kama nimekuelewa vizuri, hii sio shida sana kwa mimba kutoka miezi mitatu ya kwanza, asilimia kubwa ya kisababishi ni chromosomal abnormalities, mwili unakuwa umeona kuna shida juu ya kiumbe kilichopo na kuamua mimba itoke ili isilete kiumbe cha ajabu, (so mostly is a protective mechanism).
Lakini pia kuna vitu vingine kama maambukizi kama hayo ya Rubella, syphiliis, toxoplasmosis, cytomegalovirus, na Hepatitis.
Pia vitu kama antibodies (antiphospholipids antibodies) huweza kuwa sababu ya mimba hizi kutoka.
Kama alikuwa na Rubella probably ilikuwa inachangia kwenye shida hiyo, ila kwakuwa imetibiwa ni vyema kupima tena na kuhakikisha kuwa hana tena hayo maambukizi,
Chapili inaonekana ana shida nyingine ya mirija ambayo hii husababishwa na maambukizi kwenye njia za uzazi (Pelvic inflammatory disease) hii huweza kupelekea mirija kuziba kabisa na kusababisha asiweze kushika mimba (tofauti na mimba kushika na kutoka).
Kwa maelezo yako inaonekana hapo awali hii haikuwa shida maana aliweza kushika mimba, lakini pia kuziba mrija mmoja bado unabaki mnoja na huo uliobaki unaweza kusafirisha ovum na kutunga mimba.
Swali ni je Maambukizi haya yaliyosababisha mrija kuziba yalitibiwa!??
Kama hayakutibiwa yawezekana yaliendelea na kusababisha mrija wa pili pia kuziba, (NOTE:Maambukizi haya ni tofauti na yale ya Rubella na huwa hayanaga dalili nyingi za kujionyesha au huchelewa kujionyesha)
Na hayo maumivu wakati wa siku zake (dysmenorhoea) moja ya visababishi ni haya maambukizi yani PID,
WHAT TO DO!
Mrudi hospital bila kuchoka maana shida yenu haitibiwi kwa mkupuo, inatibiwa kwa process, inahitajika mfanye Ultrasound tena kuona viashiria vya PID na vikiwepo atibiwe vizuri pia mtapaswa kurudia HSG kuona hali ya mirija, kwakuwa hormone zilikuwa sawa na assuming hamjatumia dawa zozote za ki-hormone hii kwasasa sio ishu,
Baada ya hayo mtapaswa kupata muda wakujaribu kutafuta mtoto haswahaswa kwa kuzingatia zile siku nzuri kwenu kwenye kalenda (ni jambo zuri kuwa siku zake hazibadiliki hovyo)
Majibu ya Vipimo pamoja na matibabu ya vitakavyobainika yatadetermine nini kifuate.
Nakutakia kila laheri