Mimba nje ya kizazi

kevin strootman

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,077
1,728
Nataka kujua sababu za mimba kutunga nnje ya kizazi, tatizo inakua ni mbegu za mwanaume au mwanamke ndio mwenye shida kwenye kizazi?

Pia kama ikitunga nnje ya kizazi matibabu yapi yanatakiwa kufuatwa Ili kuondoa hilo tatizo?
 
Ectopic pregnancy inasababishwa na vitu vingi mkuu hazihusiani na mbegu za mwanamme
 
319717353_852600476186900_7743022686910428079_n.jpg

JE, UNAJUA CHANZO NA DALILI ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)?

Katika wajawazito 100, mmoja anaweza kuwa na tatizo la kupata mimba nje ya kizazi. Hali hii humaanisha kwamba, yai lililorutubishwa tayari limeshachomekwa katika tishu nje ya mfuko wa kizazi(uterus) badala ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus). Yai hili huendelea kukua ndani ya kiini tete(embryo) ambapo limeshapachikwa.

NUKUU: Mara nyingi mimba zinazotunga nje ya kizazi huwa haziwezi kukua mpaka mwisho wa ujauzito, na hivyo huweza kuleta hatari kwa afya ya mama hasa pale inapopasuka na kuvujisha damu tumboni mwa mama.

Je, Mimba Za Nje ya Kizazi Zinatokeaje?

Kwa kawaida mbegu ya mwanaume na yai la mwanamke hukutana katika mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na hapo ndipo mimba hutungika. Kiinitete husafri polepole kwenda kwenye mji wa uzazi ambako hujipandikiza kwenye ukuta wa uzazi na mimba huanza kukua. Katika ugonjwa huu wa mimba kuwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) mbegu za mwanaume na yai la mwanamke huungana ili kutengeneza kiinitete. Badala ya kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, kiinitete huenda kujipandikiza sehemu nyingine tofauti na mji wa uzazi.

NUKUU: Kinaweza kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi, kifuko cha yai(ovary), kwenye shingo ya uzazi na ndani ya tumbo la uzazi (abdominal cavity). Mimba nyingi za nje ya kizazi hujipandikiza kwenye mirija ya uzazi ambapo huwa na hatari ya kupasuka kadri mimba inavyokua. Mara chache sana mimba zinazotunga nje ya kizazi huweza kukua mpaka mwisho, nyingi huishia kupasuka na kuondolewa kwa upasuaji.

Je, Nini Husababisha Mimba Kutunga Nje ya Kizazi?

Zifuatazo ndio baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa mimba kutunga nje ya kizazi kwa baadhi ya wanawake.

• Umri wa zaidi ya miaka 40 kwa mwanamke

• Kutoa mimba zaidi ya mara 3

• Upasuaji wa mirija ya uzazi mara unapokuwa na tatizo

• Maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi(yaani PID)

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kufuatia wiki kadhaa baada ya kukosa siku zako za hedhi, basi mwanamke unaweza kupatwa na dalili kama hizi zifuatazo:

• Kuchelewa kuingia katika kipindi cha hedhi

• Kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kiuno, ambayo yanaweza kuwa upande mmoja.

• Maumivu yanaweza kuja na kuacha, au kuwa makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia.

• Kutokwa damu ukeni hasa baada ya tendo la ndoa, na mara nyingi inaweza ikatoka kidogo kidogo.

• Damu inaweza kuwa nyepesi au nzito nyeusi.

NUKUU: Wakati mwingine unaweza usipate dalili zozote, tatizo likagunduliwa wakati wa kipimo cha ultrasound. Kuna baadhi ya watu wanaweza wasipate dalili zozote na mimba kukua nje ya kizazi mpaka wakati wa kujifungua kukaribia.

Je, Unahitaji Kuondoa Visababishi Vya Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi?
 
Back
Top Bottom