MIllioni 150 za tumika kukarabati nyumba ya mkuu wa wilaya na mtumishi.

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
Inaelekea kuna mengi Mkoa wa Pwani na hata yale cha kuchimba choo kwa Mamilioni inaelekea yaukweli.

Nyumba ya Mtumishi imepigwa plasta na kuzibwa nyufa kwa 50 Millioni na 90 Millioni ni kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa wilaya.

Source: ITV Habari.
 
please naomba more information...... Roho huwa inaniuma sasa ninapoona kodi yangu inafujwa kiasi hiki...

Nina mpango wa kuunda jopo la wanasheria wa kujitolea ili tuanze kuwafatilia watu kama hawa.......

Inabidi tunusuru nchi yetu, tukiendelea hivi wajukuu zetu watatucheka in best case scenario au watakuwa hata hawana nchi ya kuishi... yote tutakuwa tumeshaiuza
 
Mwaka unaisha kwa habari hii. Jk anateua ma dc na rc wenye kutumia wadhifa wao wa kupitisha bajeti feki ili nao wale. Lile la bagamoyo matundu ya vyoo na hili sasa. Inaonesha kabisa kuna karabati nyingi za namna hii. Na kiongozi au waziri amekaa kimya au nao picha kamili ndio ileile. Rais akikaa kimya kwa mambo kama haya, harufu mbaya itamtoka kupitia wafuasi wake. Wahusika wanapaswa kuwajibishwa kwa manufaa ya uma.
 
The story goes on! this and that of the same nature! Hazina wenyewe ndo maana it's easy to munch the public coffers calmly kama vile panya ndani ya sofa la keko!
 
hiyo hela inajenga nyumba nzima tena ya ghorofa! heheh ni mwendo wa kula kwa urefu wa kamba yako...
 
Ngeleja anasema wananchi waaminini viongozi wenu, wana nia njema na nchi hii! eti sote ni wa hapa hapa! Kwa hali hii?
 
Back
Top Bottom