Milipuko ya Lissu ni Lowasa effect


Umuone mwanamke ana mimba utake ushahidi kama amevunja bikira!!
 
Upuuzi mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umuone mwanamke ana mimba utake ushahidi kama amevunja bikira!!
Huo mfano hauna mfanano na kinachojadiliwa hapa. Kilichobaki kwa sasa tuendelee tu kutazama filamu ya Lisu na Lowasa nani atamwaga mwenzake katika kinyanganyiro cha kugombea Urais 2020.

Lakini angalizo tu, watumie njia sahihi kujinadi kwetu. Kauli za kutishana na zilizojaa upotoshaji na uchochezi hazifai kwa karne hii ya sasa.
 

Sisi wote ni watu wazima, tunajua upotoshaji na ukweli. Cdm wana demokrasia yao na wala sio dhambi mwanachama yoyote kutaka kugombea urais. Au huko ccm ni dhambi watu tofauti kugombea?
 
Toa chochote alichosema Lissu ambacho ni uwongo
 
sasa mbona wote ni mlipuko. kupinga haki na kweli ngumu sana. jpm anapangua ufisadi mtupu nao wanaleta mkakati wao uwanjani kupitia watu kama lissu et al.
 
Baadaye mtafanya anayosema lissu na kutangaza kama wenye akili sana wakati ni kinyume Chake!
 
Neno kulazimishwa lina maana pana zaidi ya jinsi unavyofikiria wewe.
1. mtu unaweza kujiuzulu wadhifa ulio nao kabla ya wakati kutokana na kutoridhishwa matendo Fulani ya mkuu wako wako wa kazi kukulazimisha kufanya kile usichokiamini.Ili uwe huru wa fikra unaamua kujiuzulu.
2.Boss wako anaweza kukulazimisha uachie madaraka kwa vile tu umekataa kutekeleza kile alichokuelekeza ufanye.Hapa ndipo tujiulize sababu za hao majaji ziliegemea wapi kati ya hizo.
 
Wakati magufuli kajisiliba kua yeye mwenyewe ndio anatakiwa kugombea mbona haukuonge upupu wote huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa mbona wote ni mlipuko. kupinga haki na kweli ngumu sana. jpm anapangua ufisadi mtupu nao wanaleta mkakati wao uwanjani kupitia watu kama lissu et al.
Tupe mifano: amepangua ufisadi wa madini kwa kuwashughulikia wahusika wakuu walioidhinisha wizi? Amepangua ufisadi wa Escrow kwa kuwakamata waliosema fedha hizo hazikuwa za umma? Sasa kumbe anawashughulikia akina nani hasa???
 

Badala ya kuja na hizi speculations za kijinga ningekushauri ujikite katika kujibu hoja za Lisu moja baada ya nyingine:

1. Hali ya demokrasia nchini ikoje? Kwa nini viongozi na wanachama wa cdm nchi nzima wanakamatwa hovyo? Je mikutano ya hadhara ni hali ya kikatiba ya vyama na kwa nini watu wakitaka kukutana wanazuiliwa? Mbona CCM was wanafanya mikutano ya ndani na nje bila kuzuiliwa?

2. Je ni kweli JPM amekuwa mbaguzi, na kuendelea kanda anapotoka yeye? Jadili hili kama lina ukweli.

3. Je ni kweli JPM ana ubaguzi wa kidini? Ni kweli ana wa favour wakatoliki?

4. Ni kweli JPM anafanya matumizi kinyume na taratibu za nchi? Ununuzi wa ndege kwa mfano, ni kweli haukufuata sheria ya manunuzi?

Nadhani nimekupa njia ya kufuata kuliko kubuni tu kuwa Lisu and lengo la Iraqis.
 
Lisu anagegeda kila mtu maana naona waali wanazidi kuomba namba kupitia JF.
 
Tofautisha kati ya Hoja na Tuhuma; hizo za Lisu ni Tuhuma sio Hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja na tuhuma huthibitishwa kwa ushahidi pasi na shaka yeyote. Lisu hawezi kujibiwa tuhuma kwa hoja. Aweke ushahidi wa majaji kulazimishwa kustaafu. Tutamuelewa otherwise asitupotezee muda wetu kwa tuhuma zisizokuwa na mashiko.

Tunaendelea kufuatilia mtanange wake na Lowasa. Ngoja tusubirie naye Lowasa atakuja na yake ipi.
 
Sisi wote ni watu wazima, tunajua upotoshaji na ukweli. Cdm wana demokrasia yao na wala sio dhambi mwanachama yoyote kutaka kugombea urais. Au huko ccm ni dhambi watu tofauti kugombea?
Ni kweli kuwa Chadema ina demokrasia ya aina yake, kwakua mwenyekiti ndiye mwenye maamuzi ya mwisho nani atagombea Urais. Ila sio kweli kwamba kila mwanachama anayo haki ya kugombea Urais. Urais ni jambo geni sana huko chadema na ni jambo geni kwa Lisu pia kwakua nia anayo lakini hajui anatakiwa kufanya nini na wapi, anaishia kuibua mambo yasiyokuwa na tija.

Sasa sijui nini ilikua mantiki ya kuitisha press conference na kutuambia tuhuma kama hizo. Sasa kama yeye mwanasheria na mbunge analia lia kwenye press je mwananchi wa kawaida naye atafanya nini. Inavyoonekana shule kaenda lakini bado elimu yake haijamsaidia, kwakua hajui anatakiwa kufanya nini kwa nafasi yake kama kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa jimboni kwake.

Kuitisha press ni hatua ya kwanza kabisa ya kutafuta kiki.
 

Zaidi ya kuitisha hiyo press conference ulitaka afanyeje labda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…