Huo ni mfano unaotoka katika imani flani. Siyo udini. Ngoja nikwambie udini ni nini......
Udini ni kitendo cha mtu mwenye hadhi kama ya Lukuvi kukimbilia kanisani na kuhubiri siasa za vitisho, akitegemea Wakristo wamuunge mkono. Hii ikiwa ni sawa na kusema anawarubuni Wakristo wawatenge Waislamu ndani ya nchi moja. Maana yake ni sawa na kusema Waislamu wabaku na serikali tatu, Wakristo wakumbatie serikali mbili, ili waanze kuvutana na waislamu. Ili baadaye kukitokea machafuko ya kuhusu rasimu, iwe ni Wakristo vs Waislamu!.
Udini nikiongozi wa kisiasa kama Lukuvi kudai kukiwa na serikali tatu, Zanzibar itatawaliwa kiisalamu. Nafikiri kobe ameanza kutoa kichwa, kwani mimi naona hii ni chuki ya wazi ya Lukuvi kwa Waislamu! Kwa hiyo chuki dhidi ya Waislamu + kupeleka siasa chafu kanisani= ??
Udini ni pale chama tawala ambacho kinabeba dhamana ya usalama wa nchi kuwa ya kwanza kuanzisha siasa za kidini, kama ilivyokuwa kwa CUF Zanzibar, wakati upinzani ulipokuwa na nguvu. Baada ya kupatana mara wamekuwa safi sasa. Sasa tatizo ni CHADEMA...ni ya kikatoliki! Halafu kama vile akili zimewaganda bado mnatafuta mchawi ni nani?
Bado huelewi udini ni nini?