Mikutano mikuu ya juu CCM, iwe ya siri

Mikutano mikuu ya juu CCM, iwe ya siri

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,211
Napendekeza kila inapofanyika mikutano ya kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM na mikutano mikuu, mikutano hiyo iwe ya siri sana.Wajumbe tu waruhusiwe eneo la mikutano. Wapambe wasisogee eneo hilo.Eneo liwe na ulinzi wa kutosha.Makundi ya watu wasiohusika wasisogee wala kuwa karibu na jengo mikutano inapofanyika.

Wapiga kampeni na kadhalika wapigwe marufuku kukanyaga eneo la mikutano.Eneo la mikutano liwe la wajumbe tu si zaidi ya hapo.

Na iwe marufuku kwa wajumbe wote kuwa na simu,komputa au chombo chochote cha mawasiliano ndani ya mkutano na eneo la mkutano.

Pia wajumbe wakimaliza vikao wasiruhusiwe kuongea chochote zaidi ya msemaji wa hicho kikao husika ambaye atakutana na vyombo vya habari na kuongea nao .Hoja nzito zisilale zijadiliwe na kumalizika siku hiyo hiyo ili kutotoa nafasi ya wavuruga hoja kwenda kulala na mamluki kisha kurudi kesho yake kuvuruga hoja.

Hatua hizi ni kuepusha mambo ya vikao kuvuja wakati vikao vinaendelea
 
Wajumbe wenyewe wamegawanyika kwenye makundi,kila kundi na mgombea wake hapo unategemea siri kweli? Istoshe wajumbe wengne walishanunuliwa na UKAWA ni vibaraka wa ukawa hivyo usitegemee siri hapo kutokana na changamoto lukuki zilizopo!
 
Napendekeza kila inapofanyika mikutano ya kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM na mikutano mikuu, mikutano hiyo iwe ya siri sana.Wajumbe tu waruhusiwe eneo la mikutano. Wapambe wasisogee eneo hilo.Eneo liwe na ulinzi wa kutosha.Makundi ya watu wasiohusika wasisogee wala kuwa karibu na jengo mikutano inapofanyika.

Wapiga kampeni na kadhalika wapigwe marufuku kukanyaga eneo la mikutano.Eneo la mikutano liwe la wajumbe tu si zaidi ya hapo.

Na iwe marufuku kwa wajumbe wote kuwa na simu,komputa au chombo chochote cha mawasiliano ndani ya mkutano na eneo la mkutano.

Pia wajumbe wakimaliza vikao wasiruhusiwe kuongea chochote zaidi ya msemaji wa hicho kikao husika ambaye atakutana na vyombo vya habari na kuongea nao .Hoja nzito zisilale zijadiliwe na kumalizika siku hiyo hiyo ili kutotoa nafasi ya wavuruga hoja kwenda kulala na mamluki kisha kurudi kesho yake kuvuruga hoja.

Hatua hizi ni kuepusha mambo ya vikao kuvuja wakati vikao vinaendelea

HII NI KWENYE NCHI YENYE DEMOKRASIA NA AMANI? au tuko vitani kabisaaa? Enzi hizo zilipita mkuu, habari na taarifa za nchi kufanya siri kwa wananchi ni ushamba na ulimbukeni; Anayekosa akose peupe sio kwa hearsays na romours
 
hii yako ni positive,ebu fikiri kinyume chake?
Kingine labda utufafanulie siri hasa ni nini na je panapokutanka watu wengi pana siri.?
 
HII NI KWENYE NCHI YENYE DEMOKRASIA NA AMANI? au tuko vitani kabisaaa? Enzi hizo zilipita mkuu, habari na taarifa za nchi kufanya siri kwa wananchi ni ushamba na ulimbukeni; Anayekosa akose peupe sio kwa hearsays na romours

Kwani kazungumzia kikao cha serikali au kikao cha cha chama?weekend imeisha mkuu.
 
Kwa nini iwe hivyo? Kwani CCM inaogopa nini? Hakuna sababu ya woga. CCM ni chama kubwa au?
 
Back
Top Bottom