Mikosi na laana maarufu zaidi katika soka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
LONDON ,ENGLAND.
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Tammy Abraham amepewa jezi namba 9 ya klabu hiyo akiirithi kutoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Gonzalo Higuain.
Kwa sasa jezi hiyo inasemekana ni kama vile ina mikosi. Washambuliaji wengi wanaovaa jezi hiyo pale Chelsea katika miaka ya karibuni wamefeli. Alvaro Morata, Fernando Torres, Radamel Falcao, ni miongoni mwa mastaa ambao wamefeli katika jezi hiyo.
Kuna laana au mikosi mingi ambayo imekuwa ikihusishwa na soka.


1.AARON RAMSEY NA VIFO VYA VIGOGO.
Kiungo wa zamani wa Arsenal ambaye katika dirisha hili ametua katika Klabu ya Juventus kwa uhamisho wa bure. Ramsey alijulikana na mkosi wake wa kufunga mabao ambayo yaliambatana na vifo vya watu wengi maarufu. Mwanamuziki maarufu wa kike duniani, Whitney Houston alifariki mwaka 2012 saa chache baada ya Ramsey kuisaidia Arsenal kuichapa Southampton. Lakini pia Mwigizaji maarufu, Alan Rickman alifariki siku moja baada ya staa huyu wa Wales kuiwezesha Arsenal kuichapa Liverpool. Miongoni mwa watu wengine maarufu ambao walifariki baada ya Ramsey kufunga mabao yake ni pamoja na Steve Jobs, Osama Bin Laden, Muammar Gaddafi, Rubin Carter, Paul Walker, Robin Williams na David Bowie.



2.JEZI NAMBA 9 YA CHELSEA

Abraham aliyekulia katika kikosi cha vijana cha Chelsea ana kazi ngumu ya kuondoa mkosi katika jezi namba 9 ya Chelsea. Sio jezi nzuri kuikimbilia ukizingatia washambuliaji mahiri wanakwenda pale na sifa lukuki lakini wanashindwa kuonyesha makali yao wakivaa jezi hii. Gonzalo Higuain licha ya makali yake lakini alifunga mabao matano tu na jezi hii kuanzia Januari mwaka huu.
Kabla ya hapo mastaa wakubwa kama Alvaro Morata, Fernando Torres, Radamel Falcao na Mateja Kezman wote walivaa jezi hii lakini bila ya mafanikio yoyote. Abraham amezungumzia kuhusu mkosi huo kwa majigambo makubwa huku akisema: “Nimesikia upuuzi kuhusu jezi namba 9. Niko hapa kucheza soka langu na kujaribu.


3.MKOSI WA KUPIGA PICHA NA DRAKE.
Mamilioni ya mashabiki wa muziki duniani kote wanatamani kupiga picha na rapa maarufu wa Canada, Drake.
Hata hivyo, kwa sasa watu wameanza kujifikiria mara mbili kupiga picha na Drake. Imeibuka tabia ambapo kila unapopiga picha na rapa huyu unaelekea kushindwa katika mchezo unaoshiriki. Mastaa wengi wa soka wamejikuta wakichemsha katika hili na mmojawapo ni kiungo wa Manchester United ambaye alipiga picha na Pogba saa chache kabla ya Manchester United haijachapwa na Wolves 2-1 Kombe la FA.
Staa wa Arsenal, Pierre Emerick-Aubameyang ni mhanga mwingine ambaye alipiga picha na Drake dakika chache kabla Arsenal haijachapwa na Everton. Bondia maarufu wa Uingereza, Anthony Joshua naye alifanya kosa hilo kwa kupiga picha na Drake na kudundwa na bondia kutoka Mexico, Andy Ruiz. Wakati akipiga picha hiyo Joshua alionekana kukejeli mkosi huo lakini alijuta baadaye.




4.MIZIMU YA WARUMI BIRMINGHAM.
Inadaiwa Uwanja wa Soka wa Klabu ya Birmingham City ulijengwa katika ardhi ya mizimu ya Kirumi. Inadaiwa Klabu ya Birmingham imekuwa na mikosi mingi. Msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu uliiona timu hiyo ikishuka daraja. Katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia jukwaa lao kubwa liliungua moto. Winga wa zamani wa Birmingham, Barry Fry alijaribu kuukomboa uwanja huo kutoka katika mikosi kwa kutumia fomula yake binafsi. “Tulimuita mtu mmoja aje kuondoa mikosi katika uwanja huo na akatuambia kuwa njia pekee ya kuondoka mikosi katika uwanja huo ilikuwa kukojoa kila pembe ya uwanja. Mimi sio mtu ninayeamini mambo hayo lakini baada ya miezi mitatu nilikuwa tayari kujaribu kitu chochote kile kwahiyo nilikwenda na kukojoa katika kona zote za vibendera. Ilinichukua muda. Haikuwa rahisi.”



5.PAKA ALIYEUAWA KLABUNI RACING.
Klabu ya Racing ya Argentina ilikuwa moja kati ya klabu zenye mafanikio katika Bara la Amerika Kusini miaka ya 1960. Lakini baada ya kutwaa ubingwa wa Mabara wa Amerika Kusini na Kombe la Intercontinental mwaka 1967 kila kitu kilibadilika. Inadaiwa hili lilitokana na kundi la mashabiki wa timu pinzani ya Independiente kuvunja geti na kuingia Uwanja wa Racing na kufukia paka saba waliouwawa.
Kwa muongo mmoja uliofuata miaka ya 1970 klabu hiyo haikuchukua taji lolote. Mbaya zaidi Racing ikashuka daraja mwaka 1983. Kwa hiyo ili kukomesha laana au mkosi huo, Racing iliamua kufukua na kuwaondoa paka hao marehemu lakini waliweza kuondoa mizoga sita tu.
Mwaka 1998 Racing ilitangazwa kufilisika na mwaka mmoja baadaye ilimuita mchungaji kwa ajili ya kufanya maombi. Iliichukua Racing mpaka mwaka2001 kurudi katika hali ya kawaida na mwaka 2002 ilichukua ubingwa wa Argentina kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966.



6.JEZI NAMBA 7 KLABUNI MANCHESTER UNITED.
Sio tu Chelsea ambao wanaonekana kuwa katika mkosi na jezi namba 9. Pale Manchester United jezi namba 7 imeanza kuonekana kuwa tatizo baada ya kutamba kwa muda mrefu klabuni hapo.
Wakongwe kama Bryan Robson, David Beckham, Cristiano Ronaldo na George Best waliivaaa jezi hii kwa mafanikio. Lakini tangu Cristiano Ronaldo aondoke katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2009 jezi hiyo ni kama vile imeachiwa mkosi na laana.
Mastaa wengi waliovaa jezi hiyo wameishia kutukanwa na mashabiki. Wanakuja Old Trafford wakiwa mastaa wakubwa lakini wanachemsha vibaya klabuni hapo. Baadhi yao ni Michael Owen, Alexis Sanchez, Memphis Depay na Angel Di Maria. Wakati fulani staa wa kimataifa wa Ecuador, Antonio Valencia alikacha.



7.MZIMU WA BAYER LEVERKUSEN.
Katika miaka ya 1990 na miaka ya 2000, Klabu ya Bayer Leverkusen ilijulikana kama ‘WANAUME WANAOKARIBIA’ kutokana na tabia yao ya kukaribia makombe lakini wanaambulia patupu.
Wengine waliwatania kwa jina la the Neverkusen Men. Miaka ya 1997, 1999, 2000 na 2002, Bayer Leverkusen ilimaliza katika nafasi ya pili Bundesliga. Mwaka 2000 ilihitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa wa Ujerumani lakini ikaambulia patupu.
Miaka miwili baadaye ilipoteza uongozi wa pointi tano ambazo zilikuwa zinawapeleka katika ubingwa lakini ikapoteza mechi mbili kati ya tatu za mwisho na hivyo kuiruhusu Borussia Dortmund kutwaa ubingwa. Huo ndio mwaka ambao staa wa kimataifa wa Ufaransa, Zinedine Zidane alifunga bao la ushindi nchini Scotland katika pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Ukiwa Leverkusen wenyewe wanaamini kwamba hii sio bahati mbaya ya kawaida. Wanaamini kuna laana ambayo inawatafuna.
Hawaijui.



8.MZIMU WA GUTTMANN NA BENFICA.
Hii ni moja kati ya laana maarufu katika soka. Kocha maarufu wa zamani wa Hungary, Bela Guttmann aliondoka Porto mwaka 1959 na kujiunga na wapinzani wao maarufu Benfica. Mara baada ya kujiunga na klabu hiyo ilitwaa mataji mawili mfululizo. Baada ya kutamba katika soka la ndani la Ureno, Guttmann pia alikomesha utawala wa Real Madrid kwa kutwaa ubingwa wa Ulaya. Mara baada ya mafanikio hayo aliomba klabu hiyo imuongezee mshahara kutokana na pato la klabu hiyo kukua lakini katika namna ya kushangaza klabu hiyo ilimwambia HAPANA.
Hapo ndipo Guttmann alipoweka laana kubwa kwa klabu hiyo ya Ureno huku akisema:
“Sio kwa ndani ya miaka hii mia, kuanzia sasa Benfica kamwe haitatwaa ubingwa wa Ulaya.”
Ni kweli. Ni nusu karne sasa Benfica bado inasubiri ubingwa wa Ulaya. Ilipoteza fainali za Ulaya miaka ya 1963, 1965 na 1968 baada ya Guttmann kuondoka klabuni.


Chanzo:Gazeti laMwanaspoti
 
Ramsey kahamie Juve,, msimu wa kwanza tuu mzee wetu Sarri anaumwa, Namuomba kocha msaidizi asimpange Ramsey aisee... sisi wa Chelsea tunampenda sana sarri na ile sarriball yake
 
Tammy Abraham anafanya vizuri tu apo Chelsea

Goli nne - mechi nne ..sio mbaya

Yeye ata ondoa iyo gundu ya namba 9 apo darajani..

Kila la kheri Chelsea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom