Mikopo ya riba ndogo na mashart nafuu ndani ya siku3

Duh hizo riba hatari sana kidogo nizimie kubwa mnno nyie kweli mtakua mmepata kibali cha BOT?manake wangewaregulate kwa mujibu wa sheria wasingekubali muwakamue wananchi hivyo
 
30% ndo riba ndogo? Aisee
ulitaka upewe riba kiasi gani kwa marejesho zaidi ya mwaka mzima? Ni taasisi gani ya kifedha umewah kupewa riba chini ya 30% kwa marejesho hadi ya miaka miwili Na miezi sita? Tena ukapata mkopo haraka bila hata yakua Na acount katka campuni hiyo kwamiez isio pungua miwili au mitatu!!
 
Kwa hiyo kama nipo Arusha nahitaji huduma nakuja ofisi yenu Mbezi shule, mkabala na sheli ya Puma....nice.

Tuna offisi zetu Arusha. Clock Tower Floor ya kwanza. Utaona tangazo la VKP Investment. Wambie umeagizwa Na Madam Anneth.au ukifika hapo piga sim
 
Hivi bank sio taasisi za kifedha? Mikopo 5years riba 18%.....anyway kazi njema
 
12
%
 
Riba ni ya kawaida na nafuu..watu wengi hawana uelewa wa ukokotoaji riba na hakika ungesema unatoza riba ya asilimia 3 kwa mwezi wangejaa humu na mngesumbuliwa kweli bila kujua kuwa hiyo ni ghali sana ..yaani asilimia 36 kwa mwaka mmoja...taasis nyingi sasa zinatoza 4 percent kwa mwezi ambayo ni karibu asilimia 48 kwa mwaka...ndiyo wengi wanakwama
 
Tanzania hakuna kitu kinaitwa riba nafuu. Obasanjo alishawahi kushangaa riba kubwa za mabenki tanzania. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa alisema faida ni kubwa kuliko ya biashara ya madawa ya kulevya.
 

Hivi umelisoma vizuri tangazo?

Kuna mahali aliposema hiyo 20% au 30% ni kwa mwaka?
 
Hivi bank sio taasisi za kifedha? Mikopo 5years riba 18%.....anyway kazi njema

dada japo jamaa simjui ila namtetea kwa kupinga hoja yako.. ni kwamba bank huwa hazitoi taarifa kamili ili zipate waters.. bank hazisemagi ukweli.. binafsi nilikopa nmb 8m na nikalipa 13m kwa miaka minne..

sasa ukipiga hesabu hapo ni zaidi ya 50% nililipa...
 
Swala la udanganyifu sio bank tu, kuna mtu alisema alichukua mkopo taasisi moja hivi inajulikana tu, kilichofata alikatwa mkopo kuliko muda waliokubaliana yani kama ni miaka miwili basi inaisha wao wanaendelea tu
 
Ndo mambo yanayotakiwa kueleweshwa wateja make si kila mtu ana ufahamu na haya mambo, sasa kupanic plus kununa haisaidii
 
Nadhani huyu amesahau kuwa ile 18% au 22% inayotajwa na mabenki ni kwa mwaka. Ina maana kwamba kwa miaka minne inaelekea kuwa mara nne ya hiyo, ila inapungua tu kwa sababu ya ukokotoaji unaotegemea kiasi cha mkopo KILICHOSALIA.

Mdau wa tangazo hili labda tu angewaambia wasomaji kama na yeye hizo riba ni za mwaka au ni overall kwa mkopo mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…