Mikopo ya benki yaacha vilio

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mnada mkubwa wa kuuza viwanja, magari na nyumba zilizowekwa rehani na watu waliochukua mikopo kwenye benki umetangazwa jijini Dar es Salaam, baada ya wahusika kushindwa kurejesha.
Benki ya EFC ya jijini Dar es Salaam, imetangaza mnada huo ambao utahusisha uuzaji wa magari 43 kuanzia sasa, ambazo wamiliki wake wameshindwa kurudisha mikopo bila kutoa sababu. "Tuna kazi ya kukusanya madeni na kuuza nyumba (mali zilizowekwa rehani) na watu walichukua mikopo kwenye Benki zaidi ya 10, wateja walioshindwa kurejesha mikopo yao" alisema.

Chanzo: NIPASHE
 
Attachments

  • IMG_20180423_000030.jpg
    IMG_20180423_000030.jpg
    131.6 KB · Views: 63
  • IMG_20180423_000107.jpg
    IMG_20180423_000107.jpg
    153.8 KB · Views: 68
  • IMG_20180423_000225.jpg
    IMG_20180423_000225.jpg
    191.5 KB · Views: 81
Ni kuwa makini.Lazima ujiulize kwa nini unakopa?na pia unapeleka wapi hela za mkopo,tambua asset zote ni uwekezaji ila siyo kila uwekezaji ni asset.Elimu ya uchumi ni pana na wengi hatuna.Kufa kufaana.
 
Wakati nataka kununua tipa ya mchanga{Roli} Watu walinishauri nichukue Bank kupitia Nyumba yangu, Baadae nikaona ushauri wao ni mbovu nikaachana nao, coz ukichkulia mkopo nyumba yako ile gari siyo yako ni Bank ukishindwa kulipa wanaweza uza vyote ukabaki mtu ili wafidie kingine inatakiwa ufanye kazi ili kuikomboa nyumba yako Je? Gari ikapata ajali, Tatu utafute pesa ya Bank mpaka umalize mkopo ndiyo utafute hela ya gari je? Hiyo Gari itakuwa bado ina uhai, Nilichofanya sasa niliuza Nyumba bila ushauri wa mtu nikarudi upangaji Pesa niliyopata nikanunua Gari Tipa nyingine nikanunua kiwanja kingine na leo tayari nina Nyumba nyingine nakaa kwangu na nina Gari sidaiwi na mtu maisha safi walinicheka sana sasa wananipongeza kinafiki
 
Hivi ni vip kwa wale waliokopa kwa dhamana ya kazi then baadae wakaachishwa kazi na bado madeni yao hayajaisha ,mstakabhali wao unakuaaga vp
 
Duuh mkuu wewe uko kwenye maximum level of higher risk taker

Back
Top Bottom