Wakati nataka kununua tipa ya mchanga{Roli} Watu walinishauri nichukue Bank kupitia Nyumba yangu, Baadae nikaona ushauri wao ni mbovu nikaachana nao, coz ukichkulia mkopo nyumba yako ile gari siyo yako ni Bank ukishindwa kulipa wanaweza uza vyote ukabaki mtu ili wafidie kingine inatakiwa ufanye kazi ili kuikomboa nyumba yako Je? Gari ikapata ajali, Tatu utafute pesa ya Bank mpaka umalize mkopo ndiyo utafute hela ya gari je? Hiyo Gari itakuwa bado ina uhai, Nilichofanya sasa niliuza Nyumba bila ushauri wa mtu nikarudi upangaji Pesa niliyopata nikanunua Gari Tipa nyingine nikanunua kiwanja kingine na leo tayari nina Nyumba nyingine nakaa kwangu na nina Gari sidaiwi na mtu maisha safi walinicheka sana sasa wananipongeza kinafiki