Mikopo ya Benki na Matumizi Sahihi kwa Watumishi

Huyo kaongea tu kujifurahisha unafikiri ni rahisi kuweka saving kwa mishahara hii yetu mtu una mke watoto waende shule hujalipa kodi ya nyumba hamjala wote nyie kila siku ndo maana watumishi wana madeni hayaishi ni ngumu sana kuweka savings labda kama ni bachelor au umetokea familia ya kitajiri sana
 
mwanzo tunakuwa na kaulimbukeni. ukishalizoea gari + gharama zake na kudaiwa juu. unaanza kujuta bora mkopo wako ungefanyia jambo lingine la kukuongezea kipato.
 

I think you are not getting my point, au una escape plan mambo yanapokuwa mabaya.

Chukulia mfano wa mtu aliyesomeshwa na mzazi ambaye ni mkulima, first born anapewa majukumu ya kuangalia wadogo zake, kuwaangalia wazazi na baadhi ya ndugu.

Hapo ukiharibu umeharibu pakubwa, recovery inabaki kutegemea Neema za Mungu.
 
Pia Naomba kama kuna mtu anaweza nisaidia namna ya kuacha kazi Serikalini ila nina mkopo Bank sijui inakuwaje. Natanguliza shukrani
 

Mkuu mimi nina zaidi ya miaka 10 kwenye ajira ya serikali hivyo nilishajenga kitambo tu kupitia mkopo wangu wa pili wa benki! Ule wa kwanza kama ilivyo kwa vijana wengi, nilinunulia gari (corolla kwa enzi zile, nilitisha sana).

Sema tu kuna jamaa hapo juu (bossless) ameelezea point yenye tija pia. Kuna baadhi ya watumishi wanaumia kwa sasa baada ya kukopa ili wajenge halafu kwa kutokujua, wakajenga majumba makubwa aidha kwa kuiga au kushindwa kuitafsiri ramani!

Mwisho wa siku nyumba imeshindwa kukamilika, halafu wanalipishwa deni na riba juu! Hapa lazima uuchukie ujenzi. Jambo la msingi ni kuanza na nyumba ndogo ya kawaida (ikibidi mabanda ya uwani) itakayotosheleza mahitaji ya pesa uliyokopa then unahamia kwako! Baadae ikishatulia, ndipo ujenge nyumba ya kustaafia. Mimi nilifanya hivyo na sijutii kwa hayo maamuzi yangu.
 
Sure mkuu kujenga kunamaliza hela halafu nikitathimini faida yake sioni kama ipo kwa wastani wa miaka 5 au 6 ya kwanza.
Ukiiwekeza mahali ni vyema coz itazaa. Iliyozalishwa ndio unajengea.
Sawia kabisa, jijengee kwanza msingi wa kiuchumi ndio ukajenge. Ama ninaweza kununua gari likawa ndio la kazi na hilo hilo likawa la kulia bata.
 
Nilipoanza kazi kwasababu ya maisha niliyotoka nilijibana na kuanza ujasiriamali wa kilimo cha mbogamboga, nashukuru baada ya mwaka nikasave na kufanikiwa kupata kiwanja, nikakomaa mwaka unaofata nilihakikisha napata matofali nakweli nashukuru nilipata.
Mwaka uliofata mambo yakawa magumu magonjwa na baadhi ya mambo yalinitinga. Nikaendelea tu na harakati zangu, mwaka jana nilipata hela nikaanza ujenzi rasmi now nipo kwenye lenta, nataka nimaliza kupaua then ndio niingie bank nikachukue mkopo nimalize kibanda changu.
Nashukuru mambo yangu yanaenda bila kukwama wala familia haimenyeki sana na ukali wa maisha kwa kuwa vitu kama mchele, maharage, viazi mviringo natoa shamban kwangu.

N.b; Kujenga kwa hela ya mkopo peke yake utapata tabu sana kuna mfanyakazi mwenzetu hata vitafunwa huwa vinampiga chenga alikopa jengo halikuisha pesa imeisha na maisha magumu anasubiri mkopo uishe arudi tena bank, nilipata somo.
 
My first job ilikuwa ni benki, I was very fortunate kuwa kwenye department ambayo at least it was giving some bonuses, kwa hiyo hata ukikopa, ndani ya mwezi kuna add-ons ambazo zinafidia.

Lakini jamaa zangu wengi sana walijikuta wako very fixed, hapo ni kuanza kutafuta kazi nje, mawazo kila siku, ugomvi na mabosi kuomba nyongeza za mishahara nk nk.

And then nikaja nikahamia kampuni ambayo ni Consulting, most of the companies na individuals tuna tatizo la kuitumia mikopo kwa malengo tofauti na ya awali au yale tuliyopanga, ukishabadili matumizi ya mkopo, hata marejesho yatakusumbua.

Nikajikuta kazi zangu nyingi zikawa ni kutoa ushauri juu ya matumizi ya mikopo, ila kazi ilikuwa ngumu sana, maana unakuwa rated kulingana na response za clients.
 
yaah hii nayo point, una kiwanja unaanza hata na servant kota kwanza.
 

Ni wangapi wa aina yako wenye akili hiyo?

Matumizi sahihi ya mkopo, hicho ndicho kikubwa.

Wanasema kopa kwa sababu maalumu.
 
Pia Naomba kama kuna mtu anaweza nisaidia namna ya kuacha kazi Serikalini ila nina mkopo Bank sijui inakuwaje. Natanguliza shukrani

Vumilia tu yataisha. Usikimbie tatizo. Unless otherwise uwe tayari umeshapata mahali pengine ambapo ni bora zaidi ya hapo ulipo. Ila usije ukasema lengo nikalime! Unaweza ukalima ukiwa bado unafanya hiyo kazi yako.

Nb: Najua tu salary slip itakua ina mkeka mrefu wa makato na hivyo yamekukatisha tamaa! Vumilia tu aisee! Au nenda kwa waajiri wako ukawaambie lengo lako, watakupa utaratibu mzuri wa kuacha. Huna sababu ya kutoroka.
 
Wahindi hawajengi nyumba sijui Chanika, Mapinga na huko Goba kwenu ila wao ndo mabilionea wa Wazalendo Star kutwa kukopa kopa.
#tusipangiane#
 
Sure mkuu kujenga kunamaliza hela halafu nikitathimini faida yake sioni kama ipo kwa wastani wa miaka 5 au 6 ya kwanza.
Ukiiwekeza mahali ni vyema coz itazaa. Iliyozalishwa ndio unajengea.
Inategemeana mkuu, ni namna mtu alivyojipanga na mikakati yake.
 
Hii ya saving ni uzushi mkuu ķwenye mtu ordinary,mfn unasav lak kila mwez itakuchukua miaka mingi kufanya mln 5 na muda plus thamañ ya vitu itakua imepanda.Mim nilvyoanza kaz nılîkopà nikanunua plot thaman iliyopo kwa ss nisingeweza kununua.
So far ushaur ni mzur but sio kuchukua km ulivyo koz hatuna formula moja ya maisha.
 
Umeongea ukweli mtupu
Nna ndugu zangu wanakumbana na hili tatizo..mmoja kamaliza juzi mkopo bank, ilikuwa wa miaka mitano..take home aliyokuwa anapata inasikitisha

Huu ujumbe utamfaa sana
 
I couldnt agree more...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…