Ebu fikilia kwanini ulikopa ukipata jibu utajua ndio maaana kulipa tatizo
Kiufupi hakuna mtu anayependa kukopa, alafu akatae kulipa tatizo ni kwamba unakopa ukiwa na matatizo na unapopata ile pesa uliyotegemea kulipa unakuwa bado Upo kwenye matatizo
Ndio maaana tunashauliwa unapoitaji mkopesha mtua angalia haki ya kipato chake mda huo sio kisa mnajuna tu unampa pesa hapana.
Mfano unajua kabisa miye nadaiwa na watu zaidi ya wanne sijalipa deni, au na familia kubwa ambayo kwa kipato changu ni vigumu nikakukopa pesa alafu nikakulipa kwa wakati ikiwa hiyo pesa ndio pato langu kwa mwezi au wiki
Kwaiyo unapokopesha kuwa makini pia usipendi mazoea ya kwenye pesa na mtu, kuna watu wao matatizo hayaishagi kila siku anataka akukope wewe tu wewe tu wanini uyo mtu piga chini