MIKOPO KWA AJILI YA KUTOA MIZIGO BANDARINI NA KUHIFADHI.
UTANGULIZI:
Wafanyabiashara wengi, na watu binafsi Kulingana na kipato chao, wanashindwa kutoa mizigo yao bandarini kwa sababu ya kutokuwa na pesa kwa ajili ya kulipia inapofika bandarini, na hivyo kufanya kukaa bandarini kwa muda mrefu ambapo inasababisha kutozwa gharama nyingine kubwa kwa ajili ya kuihifadhi mizigo hiyo(storage cost). Mikopo Finance Limited ambayo ni kampuni inayojishughulisha na kukopesha mikopo baada ya kuona shida ambazo watu binafsi na wafanyabiashara wanapata, imeamua kuanzisha mikopo kwa ajiri ya kusaidia kutoa mizigo bandarini na kuihifadhi kwa gharama nafuu sana.
WALENGWA:
Walengwa ni watu binafsi na wafanyabiashara ambao wanaagiza mizigo yao nje ya Tanzania kupitia bandari ya Tanzania.
TARATIBU ZA MKOPO:
Mkopo huu kwa ajiri ya kusaidia kutoa mzigo wako bandarini unapatikana kwa masharti yafuatayo:
A. Mteja awe ameagiza mzigo, na mzigo uwe umeshafika bandari ya dar es salaam.
B. Mteja awe anahitaji fedha kwa ajili ya kulipia bandarini.
C. Mzigo uwe umeagizwa kwa kufuata taratibu zote
D. Mzigo uwe halali na sio wa magendo
E. Mteja awe ameshapata clearing agent ambae atamsaidia kutoa mzigo ambae ataleta invoice ya gharama zote,
Wote wenye mizigo bandarini ikiwa ni gari, kontena au aina yoyote ya mizigo mnakaribishwa kufika katika kampuni ili kukopa pesa kwa ajiri ya kutoa mizigo yenu bandarini.
Kwa mawasiliano:
Mikopo Finance Limited
S.L.P 15297
Kariakoo, mtaa wa Likoma / Masasi
Da es salaam.
Email: mikopofinance@yahoo.com
manager@mikopofinance.co.tz
Namba za simu:
0784 264 977