Mikoa mipya ni kwa Maslahi ya nani?

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
626
Jamani hivi kweli kuanzishwa kwa mikoa 4 mipya( Katavi,Njombe,Simiyu na Geita) kuna maana yoyote ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa maeneo haya. Kuna maswali kadhaa ambayo nimekuwa nikijiuliza bila kupata majibu:

1) Kwani maendeleo kwa wananchi yanatoka mkoa tu?
2) Kwani vitu muhimu kama huduma za jamii na miundombinu haziwezi kupelekwa kwa wananchi mpaka pawepo na ofisi ya mkuu wa mkoa?
3) Tumejifunza nini kwa uanzishwaji wa mkoa wa Manyara,ina maana matatizo yote ya wananchi wa Manyara yamemalizwa na ofisi ya RC?
4) Kuna mikoa ya pembezoni kama vile ya kusini bado miundombina ni tatizo, kwa nini tusishughulike kumaliza matatizo haya kwanza?
5) Hivi inawezekana vipi kupata makuu kutoka Katavi ambayo imezaliwa na baba Rukwa mwenye matatizo lukuki?

Nionavyo mimi, hapa kuna kamchezo tunachezewa waungwana.

Nawasilisha....
 
Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,576
1,091
Mkuu naungana na wewe, hakuna masilahi yoyote yale kitaifa zaidi ya kisiasa. Kuongeza Makada wa CCM wataoratibu kwa karibu uchakachuaji kuliko kumuachia mtu mmoja eneo kubwa. Haya yote ni matatizo ya katiba yetu inayompatia mtu mmoja madaraka ya umungu mtu. Kwa wale tuliosoma Siasa wakati tukiwa shuleni, kama mnakumbuka 1972 kulikuwa na madaraka mikoani ( decentralization). Je he tujitathmini ni kweli kuwa mikoa na wilaya inamadaraka ya kufanya maendeleo na shughuli kuwa kujiamini bila Amri ya Ikulu-Wizara etc?. Nyerere aliliona hilo wakati wa chama kimoja kuwa unapowaweka watu kufanya kazi kwa maelezo yako wanakuwa hawana uhuru wa kuamua mambo muhimu locally bila kupata baraka zako kwa woga wa kuenguliwa wakikosea.

Umefika wakati sasa katiba iweke wazi kuwa wakuu wa mikoa na wilaya wafutwe tuwe na magavana wanaochaguliwa na wananchi katika maeneo yao. Federation ni njia pekee ya kupeleka maendeleo kwa wananchi na siyo kuigawagawa nchi katika vimikoa vodogodogo na kuwapatia nyumba ndogo zetu au maswahiba wetu wa kisiasa nafasi za ulaji. It is a total waste of tax payers money. Mkoa mmoka unakuwa na Mkurugenzi wa halamashauri, mkuu wa mkoa, katibu tawala wa mkoa ukiangalia wote hawa ni redundant katika kuleta maendeleo zaidi ya kufanya kazi za chama.
 
Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
626
Boss ukizungumzia muundo wa utawala hapo ndo napata kichefuchefu kabisa na ndio maana sikutaka kuliweka hapa.
Ukiachana na huo upuuzi wa mkoani, hebu angalia wilayani. Kuna Mkuu wa wilaya,kuna sijui katibu tawala,kuna kurugenzi wa halmashauri,kuna meya nk. Kimsingi ukiniuliza mimi mwananchi wa kawaida nashindwa kutofautisha kazi zao. Hivi ni kwanini tusibaki na mkurugenzi pekee ambaye ni mtaalam aongoze asaidiane(aongoze) wakuu wa idara mbalimbali pale halmashauri kuwaletea maendeleo wananchi? Hao maDC, maRC,sijui makatibu tawala futilia mbali huko.

Ikiwezekana tuwe na kanda(majimbo) machache kama vile kanda ya mashariki,magharibi,kati nk. ambapo ndipo pawe kama hiyo mikoa.Hii itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya serikali.Na kwa mtazamo wangu,naona tutapata kanda zenye maedeleo zaidi ya huu utitiri wa mikoa kama kama ilivyo baraza letu la mawaziri.
 
Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,912
1,126
Mi Naona ni Jambo zuri ktk sera ya kupeleka madaraka mikoani (Local government) maana kupeleka madaraka karibu zaidi na watu kutasaidia kuleta maendeleo zaidi. Hiyo Mikoa Kabla Ilikuwa Mikubwa Sana Hivyo Kuudumiwa ilikuwa ni vigumu kutokana na ukubwa wake lakini tatizo hapa ni usimamizi tu hii sera ya kupeleka madaraka mikoani je unazingatia malengo ndio tatizo kubwa zaidi.
 
Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
626
Ni kweli kila mtu angependa kuwa na madaraka karibu yetu,lakini ni wazi kwamba hiki kitu hakina maana tena. Kwani hao watu wenyewe wanaosimamia hayo madaraka yetu wanawajibika Magogoni sio kwetu. Lakini pia kama utekelezaji wa hii sera umeshindikana,kuna maana gani kwetu kuendelea kuanzisha mikoa mipya kila awamu ilhali hata ile iliyopo mingi ni dhofle bin hali?

Mimi nadhani tujitathmini upya.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Jamani hivi kweli kuanzishwa kwa mikoa 4 mipya( Katavi,Njombe,Simiyu na Geita) kuna maana yoyote ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa maeneo haya. Kuna maswali kadhaa ambayo nimekuwa nikijiuliza bila kupata majibu:

1) Kwani maendeleo kwa wananchi yanatoka mkoa tu?
2) Kwani vitu muhimu kama huduma za jamii na miundombinu haziwezi kupelekwa kwa wananchi mpaka pawepo na ofisi ya mkuu wa mkoa?
3) Tumejifunza nini kwa uanzishwaji wa mkoa wa Manyara,ina maana matatizo yote ya wananchi wa Manyara yamemalizwa na ofisi ya RC?
4) Kuna mikoa ya pembezoni kama vile ya kusini bado miundombina ni tatizo, kwa nini tusishughulike kumaliza matatizo haya kwanza?
5) Hivi inawezekana vipi kupata makuu kutoka Katavi ambayo imezaliwa na baba Rukwa mwenye matatizo lukuki?

Nionavyo mimi, hapa kuna kamchezo tunachezewa waungwana.

Nawasilisha....

Ukitambua kwamba service delivery ni miongoni mwa mambo ya msingi ya utawala bora na kusogeza huduma karibu na wananchi na ukitambua kwamba nchi yetu ni kubwa sana na management yake ni ngumu, utajua kwamba uamuzi wa kuongeza mikoa ulikuwa na umuhimu wake na zoezi hili limekuwa likifanyika toka baada ya uhuru. Ndiyo maana sasa mikoa zaidi ya ishirini kutoka mikoa nane tuliyorithi wakati wa uhuru.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom