Mikoa inayotumia grid ya Taifa ya umeme yakosa umeme, grid ya taifa imesumbua Kidogo

Hizo mbwembwe tu

Kigamboni huko umeme unakatikakatika kama una kiuno vile........

Kila.leo low voltage...
In fact huku umekatika kwa zaidi ya masaa 24 mpaka sasa hivi! Tangu jana saa mbili usiku mpaka sasa hivi saa mbili usiku hamna umeme!
Maji yanategemea kupandishwa na umeme, no umeme no maji, katika mashirika ambayo ningekuwa na uwezo wa kuyafuta tanesco wangekuwa wa kwanza.
 
In fact huku umekatika kwa zaidi ya masaa 24 mpaka sasa hivi! Tangu jana saa mbili usiku mpaka sasa hivi saa mbili usiku hamna umeme!
Maji yanategemea kupandishwa na umeme, no umeme no maji, katika mashirika ambayo ningekuwa na uwezo wa kuyafuta tanesco wangekuwa wa kwanza.
Niliambiwa huko toka jana hakuna umeme

Na ninachowapendea tanesco walaa hawana presha aisee.....

Hata kufikiria kuwa huo ni mji unaokuwa kwa kasi watoe huduma ya kujitosheleza hawafikirii hivyo

Imagine hela yako unatoa na huduma hupati bila maelezo ya msingi ... (maana hadithi ya low voltage ishakuwa chukizo masikioni)
 
Resilience planning ya Tanesco imekaa vipi je kuna proper plan B, power outage inachukuwa muda mrefu katika national grid kiasi hiki? ingekuwa nchi zilizoendelea wangelipa damages kubwa sana
 
TANESCO
Tunaomba radhi wateja wetu
Imetokea hitilafu gridi ya taifa na kusababisha umeme eneo lote la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa kukosa umeme.

Tatizo hili linashughulikiwa na umeme utarudi baada ya muda mfupi

=======

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRIDI YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa majira ya Saa 12:30 imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na kusababisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Jitihada zimefanyika ili kurejesha umeme na baadhi ya Mikoa imeshaanza kupata huduma ya umeme

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

25/10/2017
mbona siku hizi umeme unakatika katika na hasa mbeya nauliza ni hujuma?
 
Back
Top Bottom