Mikataba ya Madini inasemaje kuhusu michanga ya dhahabu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Mikataba tuliyoingia na makampuni haya ya kigeni juu ya uchimbaji wa madini inasemaje kuhusu hii michanga ya dhahabu/madini?

Raisi amepewa details za mikataba hii kabla ya kuchukua maamuzi haya?

Wale wote wanaopongeza uamuzi huu bila kutafakari, Kesho na keshokutwa hawawezi kusema Raisi alishauriwa vibaya?

Kama tulikosea kwenye mikataba,hawa jamaa wakienda mahakamani tutadaiwa mabilioni mangapi ya dola kwa kusitisha usafirishaji wa michanga hii?

Kama tatizo si mikataba bali ni wizi wa makusudi tu,kwanini spika ndio sasa ameongelea swala la kuunda kamati kupitia upya mikataba hii ya madini?

Kama tulikosea kwenye mikataba na sasa ndio tunajirekebisha kwa style hii,tujue mahakamani hakuna siasa na mwisho wa siku sisi ndio tunaweza kujikuta tuaamriwa kuwalipa fidia ya mamilioni ya dola hawa wawekezaji.

Kama tulikosea ni bora kufanya nao negotiations kwanza kabla ya kuchukua hatua hizi unless tuna uhakika wa asilimia mia kuwa wao ndio wanavunja mikataba kwa kutuibia dhahabu kwa kuichanganya na mchanga.
 
Mikataba tuliyoingia na makampuni haya ya kigeni juu ya uchimbaji wa madini inasemaje kuhusu hii michanga ya dhahabu?

Raisi amepewa details za mikataba hii kabla ya kuchukua maamuzi haya?

Kama tulikosea kwenye mikataba,hawa jamaa wakienda mahakamani tutadaiwa mabilioni mangapi ya dola kwa kusitisha usafirishaji wa michanga hii?

Kama tatizo si mikataba bali ni wizi wa makusudi,kwanini sasa spika ndio ameongelea swala la kupitia upya mikataba hii?

Kama tulikosea kwenye mikataba na sasa ndio tunajirekebisha kwa style hii,tujue mahakamani hakuna siasa na mwisho wa siku sisi ndio tunaweza kujikuta tuaamriwa kuwalipa fidia ya mamilioni ya dola hawa wawekezaji.

Kama tulikosea ni bora kufanya nao negotiations kwanza kabla ya kuchukua hatua hizi unless tuna uhakika wa asilimia mia kuwa wao ndio wanavunja mikataba kwa kutuibia dhahabu kwa kuichanganya na mchanga.
Mikataba haisemi chochote kuhusu mchanga.mchanga unachukuliwa kama vile machicha baada ya kutengeneza pombe ni ya kumwaga tu.
Ndio maana mchanga ukipelekwa nje hatulipwi kwa sababu hakuna anaejua kimetoka kitu gani baada ya kuchakatwa na kina thamani gani.
Kwa nini uogope kushitakiwa wakati sie ndio tunatakiwa tushitaki kwa kuibiwa mchanga miaka yote hii 20 ya kuchimba dhahabu
 
Kwa nini hatujifunzi kwenye Historia?
Kuanzia Utaifishaji wa Mali kwenye azimio la Arusha, kisha tukawarudishia wenye mali Kwenye awamu ya 2.Kwa nini tusianzie na mikataba Kwanza, bila hata matamko? Biashara ni mapatano, siyo Matamko..
 
Nikikumbuka samaki wa Maghufuli hata hua sina hamu na maamuzi ya huyu jamaa, Mungu nisamehe bure
Kuna kitu hukielewi kuhusu samaki wa magufuli na siwezi kiandika hapa sababu ni siri ila kwa ufupi tu samaki wa magufuli ndio walimpa ujiko magufuli kuteuliwa kugombea uraisi.usilolijua ni kama usiku WA giza wewe Kama source ya taarifa za samaki wa magufuli ni magazeti jua huna taarifa sahihi .Samaki wa magufuli mtu aweza andika hata kitabu cha kurasa elfu. Mimi nilimpa kura sababu ya hao samaki wa magufuli.Muombe mungu akusamehe tu
 
Kweli akusamehe bure kwa sababu huyui kitu unafikiri yeye ndo alikuwa mwendesha mashitaka???
Mkuu huyu mtu sikama namchukia bali maamuzi yake yamewahi kuigharimu serikali billions
1. Ubomoaji wa kituo cha mafuta Mwz
2. Samaki wa Maghufuli
3. Na sasa hili LA michanga ya dhahabu. Hapa viongozi wa awamu ya tatu waliingiza nchi kwenye mikataba ya ki Mangungo
 
Madin yetu
Yako lakini huna teknolojia na mtaji uafikiri ni yako?yako ni ardhi na unayemkodishia ardhi ndio anayeondoka na mavuno. Miaka hamsini na sita ya uhuru maprofesa kibao wa siasa wanaomendea nafasi za kisiasa na uteuzi wa rais, teknologia sifuri unategemea unachako nchi hii utabaki kuangalia kwa macho tu.
 
hivi pale UDOM wale watoto wetu ci walitwaa vilaza lakini leo wale wanaonekana wana akili sana kuliko hawa ambao wanakurupuka kaltika mahamuzi,tetehe tutakula hasara mpaka watu watachanganyikiwa kama wale samaki kwa kweli
 
Mikataba haisemi chochote kuhusu mchanga.mchanga unachukuliwa kama vile machicha baada ya kutengeneza pombe ni ya kumwaga tu.
Ndio maana mchanga ukipelekwa nje hatulipwi kwa sababu hakuna anaejua kimetoka kitu gani baada ya kuchakatwa na kina thamani gani.
Kwa nini uogope kushitakiwa wakati sie ndio tunatakiwa tushitaki kwa kuibiwa mchanga miaka yote hii 20 ya kuchimba dhahabu

Mkuu kama hujui kitu usiongee kwa kujiamini kiasi hiki.
 
Mikataba haisemi chochote kuhusu mchanga.mchanga unachukuliwa kama vile machicha baada ya kutengeneza pombe ni ya kumwaga tu.
Ndio maana mchanga ukipelekwa nje hatulipwi kwa sababu hakuna anaejua kimetoka kitu gani baada ya kuchakatwa na kina thamani gani.
Kwa nini uogope kushitakiwa wakati sie ndio tunatakiwa tushitaki kwa kuibiwa mchanga miaka yote hii 20 ya kuchimba dhahabu
We jamaa boya kweli aliyekuambia mchanga hatulipwi ni Nani.Kitu kama hukijui usijifanye mjuaji
 
Utakuwa Nazi ked!!Kuna sehemu kubwa sana ya copper concentrate ipo kwenye ile michanga lakini tunapigwa
Acha bangi.Mchanga unalipiwa kabla haujasafirishwa.Hiyo kazi nimeifanya kwa mda mrefu.Madini matatu yanalipiwa ambayo in gold; silver na copper.Acha ujuaji
 
Back
Top Bottom