kilio changu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 408
- 216
Mkataba wa uvunaji wa gesi ya Mtwara na Lindi imekua siri hata kamati za Bunge zinazohusika na usimamizi zimenyimwa hiyo mikataba kwa madai kuwa ni siri na Mwekezaji ataondoka kama ikiwekwa wazi.
Najiuliza hivi hiyo mikataba inakuwa siri kwa nani?? Je rasilimali za nchi hizi ni za kina nani kama wananchi (kupitia wawakilishi wao-Bunge) wanaambiwa ni siri, sasa ni siri kati ya nani nani?? Je tuamini kuwa ni kweli siri au kuna kingine zaidi?
Je sisi kama wananchi nafasi yetu ni nini ili kuishinikza Serikali iweke huu mkataba hadharani??
Tukidharau kuhusu gesi, tutadharau katika mafuta, twaiga,pembe za Ndovu na madini yetu.
Nashauri WATANZIA ndugu zangu bila kujali itikadi yako kisiasa, bila kujali imani yako au rangi yako tuungane pamoja tuiombe serikali iweke mambo hadharani mapema kabla rasilimali zetu hazijaisha. Baba wa Taifa alipata kusema "Mjenga nchi ni Mwananchi na mvunja nchi pia ni Mwananchi" Nashauri tuchagua neno la kwanza za kuijenga nchi badala ya kuiboma nchi. Tuanze na kujua matumizi sahihi ya rasilimali zetu.
Na hiki ndio kilio changu