Mijadala ya Urais inavyolitafuna Taifa!

Mijadala ya Urais inavyolitafuna Taifa!

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
1,272
Reaction score
1,128
Taifa maskini, Taifa gonjwa, lililojaa na kunuka umaskini kila kona. Taifa lililofilisika kifikra, kiuzalishaji, na kubaki kuwa Taifa la wavivu, rushwa na ulafi.

Ndugu zangu Watanzania, na tambua na ninathamini sana mchakato wa kutafuta mrithi sahihi wa Rais Kikwete. Nikiwa nafahamu ya kwamba umakini wa kumpata mtu sahihi wakutuongoza Watanzania, nachelea kusema imetosha sasa. Tiviachie vyama vya Siasa vifanye kazi yao.

Watanzania tupo kwenye vita ya fikra. Wasomi wetu nao wameingia kwenye mtego huo. Taifa limepoteza dira na kubaki kuwa Taifa la kutabiri Raisi ajaye. Mara Lowasa, Membe, Sitta, Kigwangala naye eti anautaka. Leo naona Makinda, Migiro, Tibaijuka na Mdee! Na wengi ambao mnawajua. UKAWA nao wanataka wa kwao.

Nasema si dhambi kujadili wasaka urais. Dhambi ni kiufanya mijadala ya wasaka urais kuwa kipaumbele cha Taifa hili! Kama tumeamua kuifanya mijadala kuwa kipaumbele basi na itengewe bajeti. Na kama haitoshi tuiombee fedha kwa nchi wahisani. Nchi imesimama. Watu hawafikirii tena! Ni aibu, na kamwe hatutatoka hapa tulipo nasa.

Tumeacha kujikita kwenye msingi wa kupata Katiba Mpya na bora, tumebaki kumzungumzia Lowasa. Katiba itadumu miaka mingi zaidi ya Raisi wa miaka 5/10. Tumefumbia macho mijadala mipana ya BVR kits na mchakato mzima wa kuandikisha wapiga kura. Mchakato huu hautafanikiwa kutokana na muda uliwekwa, mahitaji na matakwa ya kikatiba yanaubana mchakato huu. Mchakato wa Kura ya maoni ya Katiba Mpya nao upo fungate. Sitaki kujikita humu lakini ni mambo ya msingi ya kujadiliwa kwa sasa na kuacha ushabiki wa wasaka urais unaotia kinyaa.

Hata kama tutapata Raisi bora kama malaika; hataweza kuifanyia lolote Tanzania kama ataongozwa na Katiba mbovu. Katiba isiyotoa dira ya kiuchumi kwa Taifa. Katiba iliyopitishwa kwa ushabiki wa vyama/kisiasa. Katiba yenye utata kwenye Elimu, Afya na Muundo wa kiutawala (serikali mbili, Tatu au moja). Katiba isiyo na maridhiano haitatupeleka popote hata kama Raisi mnayempigia chepuo Leo akawa mchapa kazi kiasi gani!

Tuyajadili hayo tukisaidiwa na wanasheria wetu huku tikiwek ushabiki wa vyama pembeni kuliokoa taifa hili linalowafanya viongozi na watumishi wa serikali kuwa na kiburi kwenye tume ya maadili. Tujenge hoja za kufuta vyeo vya wakuu wa wilaya ( lethal political posts). Je, wakurugenzi hawatoshi na wakuu wa mikoa?! Tujadili namna ya kuifanya Elimu yetu kutoka kuwa competence based/student centered na kwenda kwenye Field Based. Tuhame kumpima mwanafunzi kwa mitihani tu. Bali tumjenge na namna atakavyokabiliana na soko la ajira na kujiajiri. Kumpeleka jeshini pekee hakutamsaidia maana hata viongozi wetu wa Leo wamepitia jeshini lakini tupo hapa tulipo na tulivyo kwasababu yao. Jeshi halituletei wazalendo bali majambazi wa kesho. Jambazi kwa maana halisi ya tunayoyaona sasa. Vijana wetu wanagoma/wanaandamana kwa kuwa hata walivyokuwepo jeshini waliambia kazi zinapatikana Posta, Tigo, NSSF, UN, n.k Hawakuambiwa Nehemeia Mchechu angewapa mashine za kufyatulia matofali na kutengeza pesa.

Vijana wa Tanzania tuukwepeni mtego wa kujadili wasaka tonge. Huyo unayemsimamia na kumjaza utukufu wa kuongoza nchi atakukimbia pale adhma yake itakapotimia. Nasema kazi ya kuwaandaa, kuwapamba na kuwakashifu wengine kwa kuona wa kwako anafaa sana tuviachie vyama vya Siasa. Ni jukumu lao kwa mujibu wa Katiba mama na Katiba za vyama vyao. Tujikite kwenye mijadala yenye tija kwa Taifa na ambayo itamsaidia huyo unayemtaka awe Raisi.

Na Goodluck Mshana
 
Ni kweli tunapaswa kuwa werevu kuliko nyoka dhidi ya wasakatonge.. Vinginevyo ni kutumika kama koleo kunufaisha watu wachache...ballot box tuitumie kama sauti yetu kuliko kulalamika...mfumo uliopo unahitajika mabadiliko yasiyo na chembe ya unafiki na ushabiki wa kisiasa
 
Best post so far tangu mwaka huu uanze.you have said well Brother..huo ndio ukweli maana humu ndani masuala muhimu ya kitaifa hayajadiliwi kila mtu anaongelea uraisi tuu..hii ni fedheha na aibu kwa kweli...watanzania tunapenda sana simple and minor issues than dealing with critical issues.
 
Hakuna mjadala, Lowasa ndio rais ajae, Full Stop
 
Kuna nchi kama Netherlands watu wengi hawamjui hata Rais wao, unless otherwise mtu awe na shida inayohitaji amjue Rais. Nchi yao kila kitu kipo kwny system.

Huku kwetu bado tunaamini kuwa Rais ana direct impact ktk maisha yetu binafsi, nonsense???
 
Best post ever seen in this year...some of the critical matters lyk this needs to be discused critically kama kwel tuna nia ya dhati ya kulipeleka taifa letu kwny higher level of development!!
 
ndo tatizo letu sote,ikija maada nzuri yenye mazuri kwa mustakabali wa maisha yetu huoni watu au wakiwepo wataleta kejeli!
Lakini mada za hovyo hovyo ndo watu wanajaa!
Tusubiri wagombea urahisi wapitishwe na kambi zao then tukapige kura!!
 
[Q UOTE=laki si pesa;12091073]Hakuna mjadala, Lowasa ndio rais ajae, Full Stop[/QUOTE]

Mr. laki si pesa
Still you can change your mind to the better...
 
Taifa maskini, Taifa gonjwa, lililojaa na kunuka umaskini kila kona. Taifa lililofilisika kifikra, kiuzalishaji, na kubaki kuwa Taifa la wavivu, rushwa na ulafi.

Ndugu zangu Watanzania, na tambua na ninathamini sana mchakato wa kutafuta mrithi sahihi wa Rais Kikwete. Nikiwa nafahamu ya kwamba umakini wa kumpata mtu sahihi wakutuongoza Watanzania, nachelea kusema imetosha sasa. Tiviachie vyama vya Siasa vifanye kazi yao.

Watanzania tupo kwenye vita ya fikra. Wasomi wetu nao wameingia kwenye mtego huo. Taifa limepoteza dira na kubaki kuwa Taifa la kutabiri Raisi ajaye. Mara Lowasa, Membe, Sitta, Kigwangala naye eti anautaka. Leo naona Makinda, Migiro, Tibaijuka na Mdee! Na wengi ambao mnawajua. UKAWA nao wanataka wa kwao.

Nasema si dhambi kujadili wasaka urais. Dhambi ni kiufanya mijadala ya wasaka urais kuwa kipaumbele cha Taifa hili! Kama tumeamua kuifanya mijadala kuwa kipaumbele basi na itengewe bajeti. Na kama haitoshi tuiombee fedha kwa nchi wahisani. Nchi imesimama. Watu hawafikirii tena! Ni aibu, na kamwe hatutatoka hapa tulipo nasa.

Tumeacha kujikita kwenye msingi wa kupata Katiba Mpya na bora, tumebaki kumzungumzia Lowasa. Katiba itadumu miaka mingi zaidi ya Raisi wa miaka 5/10. Tumefumbia macho mijadala mipana ya BVR kits na mchakato mzima wa kuandikisha wapiga kura. Mchakato huu hautafanikiwa kutokana na muda uliwekwa, mahitaji na matakwa ya kikatiba yanaubana mchakato huu. Mchakato wa Kura ya maoni ya Katiba Mpya nao upo fungate. Sitaki kujikita humu lakini ni mambo ya msingi ya kujadiliwa kwa sasa na kuacha ushabiki wa wasaka urais unaotia kinyaa.

Hata kama tutapata Raisi bora kama malaika; hataweza kuifanyia lolote Tanzania kama ataongozwa na Katiba mbovu. Katiba isiyotoa dira ya kiuchumi kwa Taifa. Katiba iliyopitishwa kwa ushabiki wa vyama/kisiasa. Katiba yenye utata kwenye Elimu, Afya na Muundo wa kiutawala (serikali mbili, Tatu au moja). Katiba isiyo na maridhiano haitatupeleka popote hata kama Raisi mnayempigia chepuo Leo akawa mchapa kazi kiasi gani!

Tuyajadili hayo tukisaidiwa na wanasheria wetu huku tikiwek ushabiki wa vyama pembeni kuliokoa taifa hili linalowafanya viongozi na watumishi wa serikali kuwa na kiburi kwenye tume ya maadili. Tujenge hoja za kufuta vyeo vya wakuu wa wilaya ( lethal political posts). Je, wakurugenzi hawatoshi na wakuu wa mikoa?! Tujadili namna ya kuifanya Elimu yetu kutoka kuwa competence based/student centered na kwenda kwenye Field Based. Tuhame kumpima mwanafunzi kwa mitihani tu. Bali tumjenge na namna atakavyokabiliana na soko la ajira na kujiajiri. Kumpeleka jeshini pekee hakutamsaidia maana hata viongozi wetu wa Leo wamepitia jeshini lakini tupo hapa tulipo na tulivyo kwasababu yao. Jeshi halituletei wazalendo bali majambazi wa kesho. Jambazi kwa maana halisi ya tunayoyaona sasa. Vijana wetu wanagoma/wanaandamana kwa kuwa hata walivyokuwepo jeshini waliambia kazi zinapatikana Posta, Tigo, NSSF, UN, n.k Hawakuambiwa Nehemeia Mchechu angewapa mashine za kufyatulia matofali na kutengeza pesa.

Vijana wa Tanzania tuukwepeni mtego wa kujadili wasaka tonge. Huyo unayemsimamia na kumjaza utukufu wa kuongoza nchi atakukimbia pale adhma yake itakapotimia. Nasema kazi ya kuwaandaa, kuwapamba na kuwakashifu wengine kwa kuona wa kwako anafaa sana tuviachie vyama vya Siasa. Ni jukumu lao kwa mujibu wa Katiba mama na Katiba za vyama vyao. Tujikite kwenye mijadala yenye tija kwa Taifa na ambayo itamsaidia huyo unayemtaka awe Raisi.

Na Goodluck Mshana
Very well Said Mshana and Very big up.I will use u're topic as references.Thank you,thank you so much.Topic yako iponye watu humu hasa wale waliokwisha kosa maadili
 
Back
Top Bottom