beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Wakuu,
Nimekaa nikafikiria sana mchango mkubwa wa JF katika taifa hili ambao aidha hauonekani au unapuuzwa makusudi, nikagundua ni kwa sababu wengi hawajui wanachukulia poa.
SOTE tunajua kwamba kuna watendaji waliokuwa wanajiona miungu watu ambao baada ya Magufuli kuingia madarakani 'wameisoma namba' kutokana na mada zilizoanzishwaga humu JF ambazo ziliibua madudu yao kiutendaji huko serikalini.
Hata zile taasisi ambazo zilikuwa na wapigaji zilichanwa humu na kila mtu anajua kilichotokea.
Tusikubali JF ionekane haina faida yoyote wakati tunajua sisi kwa kiwango kikuwa tumekuwa pia 'watumbua majipu'. Hatuwezi kusema kuwa kwa asilimia 100% ni matokeo ya JF kwa jambo flani lakini tunatambua kuwa suala hilo lilijadiliwa sana JF kabla ya hatua kuchukuliwa.
Sasa katika kulipa heshima Jukwaa letu pendwa, ni vyema tukawa na kumbukumbu tunduizi pasipo na rashda wala kashda..
Mie nitataja punde zile ninazozikumbuka..
Naanza na hizi;
Kuhusu Safari za nje
Tumepata kuandika na leo tunaandika tena tukimsisitiza Rais Jakaya Kikwete na washauri wake kupunguza safari za nje ya nchi kikazi wakati taifa likiwa kwenye hali tete. Licha ya misafara yake kulalamikiwa ndani na nje ya nchi kwa sababu ya kuongozana na msururu wa watendaji ambao wengine hawana umuhimu, safari hizo hazizingatii utulivu wa nchi > Rais Kikwete punguza safari za nje
Rais Magufuli alipoingia Madarakani alisitisha > Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016...
Kuhusu Salary Slip
Kulikuwa na changamoto ya kutokuwepo kwa huduma ya Salary Slip mtandaoni. MwanaJF akaleta ushauri huu > Ushauri kwa serikali kuhusu SALARY SLIP
Serikali kupitia Utumishi wakafanyia kazi: Hatimaye Utumishi wamefanyia kazi maoni ya MwanaJamiiForums kuhusu upatikanaji wa salary slip online/
Kwenye hii thread rais alishauriwa kutumia kiswahili katika shughuli zake. kitu ambacho rais Magufuli anazingatia > Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mods msiunganishe uzi huu muhimu tafadhali. Tunataka kuweka kumbukumbu sawa.