Miili ya watu saba waliotupwa mto Ruvu yatambulika

joboychali

Senior Member
Feb 3, 2017
169
85
FEBRUARY 7, 2017
Baadhi ya vijana na wazee wa Kijiji cha Mloka Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakiongea na waandishi wa Uwazi

PWANI: Miezi miwili baada ya zile maiti saba za Mto Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani hapa, mkazi wa Kijiji cha Mloka Wilaya ya Rufiji mkoani hapa, Baba, ambaye ni mzee Ally Kitimai ameibuka na kudai kuwa, wanaye watano, walipigwa risasi miezi miwili iliyopita na watu waliokuwa na bunduki kisha kuondoka na miili hivyo kutia shaka kuwa, huenda zile maiti zilizokutwa Mto Ruvu ni miongoni mwa watoto wake, Uwazi limechimba kwa kina.


Moja ya Maiti Saba iliyokutwa Mto Ruvu ikiwa imefungwa kwenye kiroba.
MAJINA YAANIKWA

Mzee Kitimai aliwataja vijana hao ambao wote ni wa kiume kuwa ni Nassoro Kitimai, Ramadhani Kitimai, Mohammed Kitimai, Mussa Kitimai na mtoto wa mdogo wake, Hassan Fundi ambapo alisema walipigwa risasi wakiwa wanarudi kijijini kutoka kuvua samaki kwenye bwawa moja lililopo kando ya Mto Rufiji kwenye Hifadhi ya Pori la Wanyama ya Selous inayopakana na kijiji hicho.

MAITI ZACHUKULIWA

Alisema baada ya kuuawa, watu hao waliondoka na miili yote mitano ambapo hawakujua ilikopelekwa mpaka leo. Waliokuwa na marehemu hao na kufanikiwa kutoroka wakati wakishambuliwa, ndiyo waliotoa taarifa baada ya kurudi kijijini.

SIMULIZI YA BABA WA MAREHEMU HAO NI HII

Akizungumza kwa uchungu na Uwazi kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita, mzee Kitimai alisema: “Suala la sisi wanakijiji kuuawa kwa kupigwa risasi tunapokwenda kuvua samaki limekuwa la kawaida mpaka kuna kipindi wanakijiji tulishawahi kuandamana ili kufika kwenye kituo kimoja cha askari kilichopo karibu na kijiji hiki lakini tulipofika kwenye geti la kuingilia tulikuta askari hao wameweka bendera nyekundu na kutuonya kuwa atakayethubutu kukanyaga eneo hilo itakuwa ndiyo mwisho wa maisha yake.”

Maiti nyingine kwenye kiroba
“Sasa wakiwa njiani kurudi nyumbani, walishtukia wakishambuliwa kwa risasi na watu waliokuwa na bunduki.Wanangu wote watano waliuawa palepale lakini kuna wenzao wawili waliweza kuponyoka na kufanikiwa kufika hapa kijijini na kutueleza kilichotokea.”

AFUATILIA MAITI

“Baada ya tukio hilo, niliona hata kama wanangu walikuwa na makosa mimi niliamua kumwachia Mungu, hivyo nilifuatilia miili yao kule walikopigiwa risasi ili niweze kuileta kijijini niihifadhi kwa mujibu wa dini yangu ya Kiislam lakini haikuwa rahisi kwani kufika eneo lile hatukuiona miili. Ina maana waliondoka nayo wenyewe baada ya kuwauwa.”
 
Hii habari haieleweki na kama zimechanganywa habari mbili tofauti. Kaandae vizuri kisha uiweke sawa. Na hicho chanzo chako cha habari magazeti ya udaku kwa kuunga unga stori kuna siku wataingia matatizoni kama lile gazeti lililoandika wizi wa kifaru cha JWTZ.
 
Serikali ilishindwa kutambua kuwa miili bi ya kinanani!! Hatuna wataala wa upelelezi.Hili jeshi ka polisi haliba tifauthi na mgambo wa alimashauri..Hupelelezi ulikuwa rahisi sana lakini wao wameshindwa.wasije kuwa wao ndio wahusika wa hayo mauaji
 
Waliowapiga risasi hao wanakijiji ni nani?,mleta uzi hebu hakiki hii habari naona kama kuna mchanganyo wa taarifa,huu unyama wa hali ya juu sana.
 
Huyo mzee aache unafiki, kama ilikuwa ni hivyo mbona hakutoa taarifa yoyote police baada ya kuambiwa na wale walionusurika?? Taarifa za ile miili zilisambaa kwa kasi sana kwenye vyombo vya habari na ulikuwa ndiyo muda muafaka wa yeye kueleza kilio chake, kwa nini alikaa kimya mpaka miili ikazikwa??
 
Mbona hii taarifa kama ina uwalakini ndani yake?ina maana mzee baada ya kuambiwa wanae wamepigwa risasi na akafatilia miili na kuikosa kwa nini hakwenda kituo cha polisi kuripoti?na je baada ya kusikia kuokotwa kwa miili mtoni kwa nini asingekwenda kujiridhisha?vinginevyo ametumwa labda abadilishe upepo wa dona..
 
Imenikumbusha kipindi nasoma makelele university miaka ya 70
wapiiii Dogo. Uliluwa A level Makongo late 2000. Anyways hongera zako na masters ya upishi (catering services)

Dah Makelele ama unamaanisha yule mjezaj mfaransa asili ya Kongo Claudio Makelele?
 
Mbona hii taarifa kama ina uwalakini ndani yake?ina maana mzee baada ya kuambiwa wanae wamepigwa risasi na akafatilia miili na kuikosa kwa nini hakwenda kituo cha polisi kuripoti?na je baada ya kusikia kuokotwa kwa miili mtoni kwa nini asingekwenda kujiridhisha?vinginevyo ametumwa labda abadilishe upepo wa dona..
police hawana ushirikiano
 
Back
Top Bottom