Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,477
- 34,521
Habari za jumapili wanagenzi.
Baada ya Tamko la Waziri wa Tamisemi kutengua waraka wake alioutoia 30/11/2016 kuhusu marufuku ya Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji kutumia mihuri kama vitendea kazi. Hali bado ni tete kwa sababu zifuatazo...
Kwa nini nimesema haya hapa.
Suala la kuwaondolea mamlaka wenyeviti ni jaribio dhidi ya Katiba na Sheria bila kujali madhara yake.
.......Rais wangu Magufuli, unazungukwa na wasaidizi wako. Unapowateua usitegemee ule utakatifu uliowaona nao kipindi cha uteuzi ndiyo wanadumu nao hadi sasa. Wengi wanajua wanachokifanya na hawatakuwa na hasara endapo mambo yatakuharibikia. Kinachofanyika sasa ni kuichonganisha serikali yako na wananchi kwa makusudi......
Nimetimiza wajibu

- Waziri ametoa tamko kwa umma kupitia media ambapo ni sahihi pia. lakini hakupaswa kuishia hapo alipaswa kupeleka waraka wa kiutendaji kwa ngazi husika ili kufuta ule waraka wa mwanzo kupitia waraka tenguzi.....
- Wakurugenzi wengi wa Halmashauri na Makatibu Tawala walifika mbali zaidi hadi kuhusu suala la Mihuri ya Wenyeviti ambapo polisi walihusishwa wasitoe ushirikiano kwa wenyeviti kupitia mihuri yao. Hivyo hadi sasa bado katazo limesimama na halijafutwa katika kada ya utendaji.
- Kitu pekee ambacho kilikuwa kinaitwa stahiki ya mwenyekiti ni posho ya mawasiliano ya Tshs 50,000/- kwa mwezi ambayo kwa mwaka mmoja anaweza akapata hiyo kwa miezi isiyozidi saba huku akipotezewa mingine, sasa imesemekana hiyo nayo imeondolewa na hawatalipwa chochote just kuhanikiza maagizo ya Waraka wa 30/11/2016 wa TAMISEMI (Ni taarifa)
- Watendaji wa Kata walio wengi wameendelea kutoa vitisho kwa Wenyeviti kwa kuwaambia mwenyekiti wa mtaa atakayetumia mhuri wake katika nyaraka zozote atakamatwa na kushtakiwa. Mfano hai ni Mtendaji wa Kata ya Keko Miburani ambaye hivi juzi amesisistiza hayo....
- Hakuna Mwenyekiti hata mmoja ambaye alirudisha Mhuri wake kwa Mkurugenzi wa Manispaa kupitia Mtendaji wa Kata aliyerudishiwa mhuri huo kwa matumizi ya kiofisi. Hakuna mawasiliano, utaratibu wala mwelekeo wa hilo kufanyika