Migogoro kwenye ndoa na utatuzi wake.....

Migogoro kwenye ndoa na utatuzi wake.....

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
20,143
Reaction score
40,910
Habari za muda huu wapendwa...moja kwa moja niende kwenye mada husika.....

Si jambo la ajabu kuona kuwa nyakati hizi ndoa nyingi zimegeuka vituo vya mateso na manyanyaso...watu wengi wanajutia maamuzi yao ya kuwa kwenye ndoa na wengine wanaishi kwenye hizo ndoa kama misukule...kwa kuwa hawana la kufanya zaidi ya kuyavumilia mateso......

Wengine wameshajitoa uhai wao baada ya kushindwa kupambana na vita vya kihisia kutokana na changamoto zilizopo kwenye ndoa.....

Lakini hebu tujiulize kwa makini haya mambo au hii migogoro na mateso kwenye ndoa huwa inatokea tu...!!?

Jibu ni hapana

Haya mambo huwa yaaanzia mbali sana isipokuwa tu wapendanao wanaamua kuyapuuzia na baadae yakija kuibuka yanakuwa makubwa na utatuzi wake unakuwa mgumu na hatimaye kupelekea watu kupata msongo wa mawazo........

Kwa kawaida ndoa huanzia uchumba na baada ya uchumba ndio watu wanaona kuwa inafaa kuwa pamoja kama mke na mume na hatimaye kufunga ndoa.......

Watu wengi hawajui lakini viashiria vingi vya usalama na furaha ya ndoa yako huwa vinajionesha kwenye uchumba na watu wengi huwa wanaamua kupuuzia wakiamini kuwa mambo yatabadilika.....

Kuna tabia za kawaida ambazo zinaweza kurekebishika kwa mwenza mwenye utayari lakini zingine ni kama ngozi ya mwili......

Kwa mfano kama mwenza wako ana tabia ya kukufokea wakati wa uchumba wenu na hata muda mwingine kufanya pasipo kuangalia faragha basi jua kuwa hiyo ni hulka yake wewe hutaweza kumbadilisha na watu hao huendelea na kuwa wanyanyasaji kwenye ndoa.....

Kama mpenzi wako wakati wa uchumba tu mmekuwa mkisuruhishwa kesi zinazohusiana na masuala ya usaliti maana huyo haheshimu uwepo wako kwenye maisha yake na kamwe hawezi kuheshimu ndoa takatifu........

Kama wakati wa uchumba mmekuwa mkizozana juu ya suala moja linalokukera wewe tu huku mwenzako akilifurahia basi hapo akili kichwani mwako........

Mambo yanayoonekana kuwa ni madogo wakati wa uchumba ndio yanayokuwa makubwa kwenye ndoa na kuinyima amani ndoa yako.......hizo basi wakati wa uchumba unatakiwa urekebishe makando kando yote wewe mchumba wako kabla hamjaingia kwenye ndoa takatifu........

~Jinsi ya kutatua migogoro ya kwenye ndoa
Migogoro ya kwenye ndoa inakuwa mizito kuishughulikia kwa kuwa inakuwa imejikita kwenye hisia sana maana yake maamuzi ya upande mmoja unaweza kuleta maafa upande mwingine......Kwa mfano kutokana na mgogoro mnaweza mkaamua waachane je hao wanandoa wanaweza kuvumiliana kuwa mbali na mwenzie hata kama waligombana..!!?

Kwa hivyo basi maamuzi yanayohusisha migogoro ya wanandoa inatakiwa hekima na busara za hali ya juu sana kuliko kughafirika.....

Ni vyema migogoro yenu mkawashirikisha watu wazima mnaowaamini ambao walishawahi kuwa kwenye ndoa au bado wapo kwenye ndoa....maana inakuwa rahisi kuwa shauri kwa kuwa wana ni hali gani mnapitia.....

Nawasilisha....
 
Kabisa nakubaliana na wewe, na pia kuomba msaada nje sio dhambi n kutaka tu kuweka hali sawa mana kuna wengine wanaona kama siri zao zinatoka nje ilhali wewe unataka kuomba msaada wa nyie wawili muwekwe sawa, halaf nguvu ya msamaha itambulike kati ya hao wachumba au wanandoa, mtu akisema samahani ieleweke ametambua makosa na anahitaj kujirekebisha, msamaha ukiombwa kwa dhati usikilizwe,msingi mzur wa ndoa yenu huanza chini huku upenzi au kwenye uchumba wenu, the way mnaishi na kusulushisha mambo yenu nimependa hapo kushirikisha watu wazima tunaowaaamini
 
Back
Top Bottom