Migogoro ktk mapenzi ina nafasi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro ktk mapenzi ina nafasi gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzalendo wa ukweli, Oct 22, 2012.

 1. Mzalendo wa ukweli

  Mzalendo wa ukweli JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 562
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajamvi, kama heading isemavyo; hivi migogoro katika mapenzi ina nafasi gani? Je inaimarisha penzi baada ya kusolve au inapunguza kiasi cha upendo kati ya wapendanao? mchango wako please!!!!!
   
 2. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Inategemea ni mgogoro wa nini, kuna mengine inapunguza penzi kwa asilimia kubwa sana ila mingine kiasi fulani inaleta upendo zaidi.
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwa asilimia kubwa, migogoro ktk mapenzi inapunguza kasi ya mapenzi. Ndoa nyingi zilizovunjika chanzo chake huwa ni migogoro. Binafsi siamini sana ktk migogoro kujenga au kuimarisha penzi, ila naamini ktk uwazi wa ndani ya mapenzi nikimaanisha kuambiwa wapi nimekosea au kumwambia mtu wapi kakosea ili ajirekebishe, heshima, uaminifu, kusaidiana na upendo wenyewe kama silaha ya kulinda mahusiano.

  Migogoro huleta chuki, huleta nyumba ndogo na vibustani, huleta kero, maudhi, majuto (Kwanini nilimuoa au kuolewa na fulani), magonjwa (stress, pressure, ugonjwa wa moyo, nk), vifo (wapo waliojiua na kuua kwa sababu ya ugomvi tu), yatima nk. Kwa kifupi sioni jambo jema saaana ktk migogoro kutumika kuimarisha mahusiano!
   
 4. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haijengi bali hubomoa...........

  c'z inachujisha penzi
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wewe unadhani ina nafasi gani?
   
 6. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Migogoro inayosababishwa na kulala na mwanamke/mwanaume mwingine mara nyingi inapelekea mapenzi kupungua kama si kuisha.

  Hii ikitokea pale mnapokuwa kwenye mahusiano halafu mwenzi wako akawa anatembea nje ni hatari kabisa. Inaua mapenzi. Ila kama mligombana kwa muda na kila mtu akaendelea na maisha yake then mkarealize kuwa mnapendana, mkarudiana basi migogoro ya kuwa ulitembea na fulani mara nyingi si ya kubomoa mapenzi. Ni kukubaliana na hali iliyotokea na kusonga mbele.
   
 7. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Migogoro hupunguza mapenzi katika uhusiano, coz saa zingine mtu anapata majeraha/misukosuko kazini, kwa marafiki au kwingineko lakini akija kwako anajua anakuja kupumzika na kurelax mpaka stress kwishiney, sasa piga picha umegombana na boss, foleni halafu mkeo/mpenzi hamuongei si unakufa kabla ya siku zako?
   
 8. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Ukishasema kuwa ni migogoro basi hilo tu Neno migogoro si jambo la kheri, kwa ujumla haina tija katika ndoa.
   
 9. Mzalendo wa ukweli

  Mzalendo wa ukweli JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 562
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani inategemea na aina ya mgogoro wenyewe na inaweza ikaimarisha upendo kati ya wawili au ikapunguza kabisa kama sio kuua.
   
 10. Mzalendo wa ukweli

  Mzalendo wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 562
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu Miwatamu migogoro/misunderstanding ktk mapenzi ni kitu ambacho nadhani hakiepukiki 7bu si mara zote mtakuwa ktk hali ya kuelewana tu zipo nyakati ni lazima kutatokea tofauti/misunderstand, sasa inategemea mnazimalizaje hizo tofauti zenu.kama zikimalizwa vizuri mara nyingi hupelekea upendo kuimarika na kukua lakini endapo mtamaliza vibaya kuna uwezekano wa kupunguza kama sio kuua kabisa upendo. Kwa Kifupi nadhani upendo ni lazima uwe tested ili kuuimarisha. mtazamo wangu
   
 11. HoneyBee

  HoneyBee JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Migogoro ni majaribio. No relationship is free of migogoro. Huwezi kusema hata siku moja hujawahi kukosana na ndugu yako hata mmoja. Mkikosana mnasuluhisha, yanaisha, maisha yanaendelea, mnasahau basi. Mapenzi hayapungui lakini uhusiano wenu unaweza ukawa na nguvu zaidi.

  Ukikumbwa na mgogoro katika uhusiano kati ya mwenza wako, penzi linaongezeka kama reaction yenu itakuwa ni la kusuluhisha mgogoro na si kuliongezea matizo mengine ambayo pengine yatasababisha matatizo mengine. Kwa mfano, mume anahisi mapenzi yamepungua kutoka kwa mke wake baada ya miaka kadhaa ya ndo. Badala ya kukaa na kuongea na mkewe kuuliza kulikoni (labda kuna stress, au mabadiliko ambayo mke wake anapitia, you know us women!), anaamua kuenda kutafuta nyumba ndogo ambayo sio solution, na inaongeza matatizo mengine kwenye uhusiano. The best people in your life are the ones that will stick with you through thick and thin. Kwa maana, mahusiano YOTE yanapitia milima na mabonde lakini mkishikana mpaka mwisho wa safari uhusiano wenu utakuwa na nguvu na upendo mwingi mno!
   
Loading...