Migodi yalalamikiwa kwa udhalilishaji, yapekua wafanyakazi maungoni

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Dodoma. Bunge limeelezwa kuwa, baadhi ya wamiliki wa migodi huwapekua wafanyakazi hadi sehemu za siri ili kubaini iwapo wameficha madini.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Joyce Mukya akiuliza swali leo bungeni alisema kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji kwa wafanyakazi wa migodini kwa kupekuliwa hadi sehemu za siri na wenye migodi.

“Kumekuwa kunafanyika udhalilishaji mkubwa kwa wafanyakazi, wamekuwa wakikaguliwa sehemu za siri hasa njia ya haja kubwa, je, Serikali inatuambia nini na inachukua hatua gani juu ya udhalilishaji huu?” alihoji Mukya.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akijibu swali hiyo alisema malalamiko hayo aliyapata katika mgodi wa TanzaniteOne hivyo wanayatambua.

Katika swali la msingi Mbunge wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu alitaka kujua ni lini serikali itafanya ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini na akahoji ni kwa nini serikali isiamue kuwaondoa nchini waajiri wakorofi jwa unyanyasaji wanaoufanya.

“Anachokisema mbunge ni kweli na nilienda kutembelea huo mgodi na nikakutana na changamoto hiyo kubwa na wafanyakazi walinieleza, kwa kweli inasikitisha sana na haipendezi,” alisema Mavunde.

Alisema alitoa maelekezo kwa sababu upo utaratibu wa kisheria wa kufuatwa wakati wa ukaguzi na kama vitendo hivyo vinaendelea, Serikali haitasita kuwachukuliwa hatua wahusika, ikiwamo kuwafukuza kama watashindwa kufuata sheria za nchi.
 
Kwa hiyo wasipekuliwe?
 
Kwa hiyo wasipekuliwe?
Mada haina maana hiyo hiyo ...soma vizuri uielewe sawa sawa!

Kila MTU anahitaji heshima ya kibinadamu na siyo kudhalilisha utu wa mwanadamu!!
 
wabongo wengi tunapenda Sana short cut zakimagumashi kufikia utajiri,kupiga kazi wengi hawapeendi.
Kunamlemavu sasa Ni tajiri yeye alikuwa akificha madini kwenye mguu wa bandia...mpaka kushtukiwa na kufukuzwa tayari keshawanyoosha vyakutosha! Unamfukuza kazi mtu anakucheka.
labda waziri aseme kama kunavyombo special vya kukagua lasivyo watu watachomeka mizigo popote
 
Back
Top Bottom