Migiro Kuigharimu Tanzania

migiro atagombea ubunge segerea, atapita kwa gharama yoyote halafu atachukua nafasi ya pinda fasta, kama huamini subiri matokeo ya segerea yabatilishwe uone muziki!

Mkataba wake unaisha Jun 2012
 
JK ameshindwa kumtumia shushushu aliyekubuhu mtoto wa mkulima atamtumiaje Migiro? Tatizo haliko kwa mawaziri, mimi lawama zote kwa "Mzee wa ahadi lukuki"-JK. Tumempa Magufuli hapa ameanza kufunga mota, anamwambia punguza spidi. Tumempa Sitta mzee wa spidi and standards kamtoa kwenye uspika. Tumempa Mwandosya, ona washikaji zake wanachomfanya. Hata aje Migiro hatafanya kitu kama JK mwenyewe hataacha kuchekacheka hapa bongo. Natamani mzee Kifimbo afufuke aje awakemee.
 
Kama huyo mama katemwa huko UN, sisi hatuna haja naye hapa. Mongela alishindwa kule Kwa Madiba, hapa alitaka kugombea uprezida tukampiga chini. Na huyo Migiro bora akaombe kazi kwa Mkandala pale UDSM tunahitaji walimu wa sheria. Au aende kule UDOM wanakotoa digrii uchwara akawasaidie. Watoto wetu wanalia kila siku kule kwamba kozi ya semista nzima wanafundishwa kwa siku tatu, eti wennyewe wanaita extreme, ujinga mtupu halafu maprofesa wako pale wanaacha tu mambo yawe hivyohivyo. JK tunajua huwa husikii, lakini piga chini mawaziri hao usimsubiri huyo Migiro wako, la sivyo mpe kazi nyingine else where sio kwenye baraza, kashindwa kazi huyo huko UN.
 
Migiro ni mama mzuri na ambaye ameondoka hapa bila matatizo yoyote. Lakini kwamba ameshindwa kazi na sasa anarudi Bongo kuja kuwa Waziri , ni jambo la kusikitisha sana. Wadhifa wote ule, mkubwa kiasi kile unakuja huku kwenye uchochoro ambako kupata hela mpaka uibe za wagonjwa na wenye njaa.
 
JK anasubiri migiro aja ampe ubunge halafu uwaziri na baadaye uraisi kwani JK ameshaona nchi hii ni mali yake hivyo na urais atamwachia anayemtaka. Sijawahi kuona mtu wa ajabu na muoga kama pinda, waziri mkuu gani ambaye hana maamuzi.........JK alishamfahamu tangu awali ndo maana ana-mpeleka kwa remote, Pinda unayejiita mtoto wa mkulima usijiite tena hivyo kwani watoto wa mkulima wana-ujasiri, umejishusha sana ulikuwa unatakiwa ujiuzulu ndo JK angejifunza. sasa wewe unaendelea kudharaulika, umebaki waziri mkuu jina tu, aibu!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…