Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako, naomba kwa heshima na taadhima nikushauri, wewe na wasaidizi wako (wataalam), juu ya umuhimu wa kuanzisha somo la uzalendo. Ambalo litaanza kufundishwa tangu mwanafunzi akiwa kwenye madarasa ya chini kabisa.
Lengo la somo hilo ni kumfanya mtoto akue huku akijua kwamba kinachopaswa kutangulizwa ni nchi yake pamoja na rasilimali zake kwanza. Elimu kwa maana ya masomo mengine kufundishwa, iendane na maakuzi ya mtoto mwenye mtazamo wa kizalendo kwa kila kinachomzunguka.
Ufisadi, hujuma dhidi ya mali za taifa, kutaka nchi yako mwenyewe ishindwe kesi, au ishindwe kwenye mechi za soka za kimataifa, hayo ni mfano tu wa mambo yenye kuelezea kwa upana ni jinsi gani ukosefu wa somo la uzalendo kwa mapana, unavyoiathiri jamii ya Tanzania.
Wapo wanaozungumzia umuhimu wa Afrika (Tanzania) kuwa na mifumo imara ya uongozi, hawa wanayo hoja tena nzuri sana lakini taasisi imara bila ya mtu kutanguliza uzalendo, ni kama pambo zuri lenye kuvutia lakini limewekwa sehemu iliyo mbali na macho ya watu.
Kwanza tuanze na somo la uzalendo, mtoto akuzwe huku akiwa na uchungu na nchi aliyozaliwa.
Tukishakuwa wazalendo ni rahisi sana kujenga mifumo mizuri ya uongozi, kwani mtu anakuwa tayari ameshalifahamu deni alilonalo kwa nchi yake, kwa ardhi ambayo imewazika babu na bibi zake.
Naamini Profesa Ndalichako utayasoma na kupima kama mawazo yangu yanafaa kufanyiwa kazi au hayafai.
Jumapili Njema.