Mgosi Mbena
JF-Expert Member
- Nov 28, 2023
- 544
- 665
Mzee umbumbumbu wetu ndio unafanya tuwaze uaminifu pekee. Nchi za wenzetu hazina watu waaminifu, zina strict legal systems tu! Ukizingua unafilisiwa na kufungwa fasta. Sisi tunataka kubembeleza watu wawe na hofu ya Mungu badala ya kuweka mifumo inayowabana wezi.Nguzo ya kwanza : UAMINIFU
Uaminifu wa watu,taasisi na jamii huongeza na kukuza uchumi kwa kuchochea biashara na ujasiria mali,
Jamii ya watu wasio waaminifu ni ngumu sana kufanya nao biashara, kuagiza mizigo,kulipia bidhaa.
Kila mtu akiwa mjasiriamali nani atamfanyia kazi mwenzake? Hiyo entrepreneurship mindset inahubiriwa kwa sababu soko la ajira limefeli, hakuna nchi iliyoendelea kwa kila mtu kuuza nyanya au genge, tunachohitaji ni kuwa na viwanda vikubwa vinavyotoa ajira rasmi na za kueleweka.MTAZAMO WA UJASIRIA MALI
Kuwepo jamii zenye mtazamo huu huchochea ubunifu na biashara! Sehemu ambayo kila mtu anawaza kuajiriwa ni ngumu sana kuwa na jamii iliyoendelea kwani hamna nchi inajengwa na Ajira tu.
Mkuu unaweza kuwa sahihiii kwa mifano unayolenga!Mzee umbumbumbu wetu ndio unafanya tuwaze uaminifu pekee. Nchi za wenzetu hazina watu waaminifu, zina strict legal systems tu! Ukizingua unafilisiwa na kufungwa fasta. Sisi tunataka kubembeleza watu wawe na hofu ya Mungu badala ya kuweka mifumo inayowabana wezi.
Kila mtu akiwa mjasiriamali nani atamfanyia kazi mwenzake? Hiyo entrepreneurship mindset inahubiriwa kwa sababu soko la ajira limefeli, hakuna nchi iliyoendelea kwa kila mtu kuuza nyanya au genge, tunachohitaji ni kuwa na viwanda vikubwa vinavyotoa ajira rasmi na za kueleweka.
KaribuUmenena
Kuna ukweli mmoja mchungu inabidi tuukubali mkuu, binadamu wote duniani tabia zao zinafanana sana, kinachowatofautisha ni mazingira na mifumo inayowaongoza.Mkuu unaweza kuwa sahihiii kwa mifano unayolenga!
Lakini angalia inchi zote zilizofanikiwa zina
Kitu kimoja in common βUAMINIFUβ hata mali ikipotea ni inapatikana
- π―π΅ Japan β exceptionally effective lost-and-found system; police receive and catalog millions of lost items.
- πΈπ¬ Singapore β organized public transport and police lost-property systems.
- π¨π Switzerland β strong lost-property systems, particularly on public transport.
- π©πͺ Germany β municipalities and transport companies operate formal FundbΓΌro (lost-and-found offices).
- π³π± Netherlands β well-organized systems for lost items, especially on trains and public transport.
- π¬π§ United Kingdom β transport operators, police, and private lost-property services handle lost items.
- π°π· South Korea β centraliz
Ha ha una point mkuuKuna ukweli mmoja mchungu inabidi tuukubali mkuu, binadamu wote duniani tabia zao zinafanana sana, kinachowatofautisha ni mazingira na mifumo inayowaongoza.
Chukua Mbongo mmoja mjanja mjanja kutoka Kariakoo, mpeleke hapo Singapore au Tokyo aishi huko kwa mwaka mmoja, unafikiri ataiba simu akizikuta zimesahaulika? Hawezi na atakuwa ni mtu mwaminifu sana pengine kuliko hata wao, kwa sababu anajua kule hakuna connection ya mjomba itakayomtoa korokoroni.
Sasa chukua huyo Mjapani unayemsifia, mtoe Tokyo mlete aishi mazingira yetu ya uswahilini ambapo umeme unakatika siku tatu, maji hakuna, na polisi ukiwafuata wanakuomba rushwa. Nakuhakikishia baada ya miaka miwili huyo Mjapani atajifunza michongo na atakuwa wa kwanza kukutapeli!
Uaminifu ni matokeo ya mazingira yanayomzunguka mwanadamu.