Mifuko ya jamii nchini inakera sana

Mifuko ya jamii nchini inakera sana

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
***ADMINS****naomba msaidie ku-edit kichwa habari kisomeke...."Kunahitajika Mjadala Mpana Kuhusu Fao La Kujitoa"....Nimeshindwa ku-edit heading


Kutokana na hali inayoendelea au sintofahamu inayoendelea kuhusiana na fao la kujito linalowaumiza wengi, mimi nikiwa miongoni mwao hao wanaoumia; ifike wakati tukubaliane kuwa, unahitajika mjadala mpana kuhusu hili la fao la kujitoa. Mjadala huo unahitajika kutokana na na kila mtu kuzungumza yake na kufanya yake.

TUCTA ambao ndiyo wawakilishi wakuu wa wafanyakazi, wamekuwa kimya na ukimya huo, umepelekea wafanyakazi ambao ni wahanga wa mafao ya kujitoa wawe wanawasilisha malalamiko yao wenyewe kwa wabunge, mbaya zaidi wanawasilisha malalamiko yao aidha nusu nusu ama kwa namna isiyowezesha wabunge kufahamu vizuri kinachoendelea juu ya hili la 'fao la kujitoa'.

Wakati naibu spika wa bunge (jana tarehe 14-11-2017) anasema hilo suala lilishakuwa closed, na wakati mawaziri wa wizara ya kazi na ajira wakisema wanashughulikia suala hili ili kutafuta namna nzuri ya kulimaliza, ukweli ni kwamba, mifuko ya jamii inafanya mambo kimzaha mzaha, ni vurugu mechi.

Mathalani, watu wanaopoteza ajira kwa kufukuzwa kazi hawapewi mafao yao wanaambiwa watafute ajira nyingine ili kuendeleza uanachama wao ili mafao hayo yaje kutolewa wakifikisha umri wa kustaafu yaani miaka 55. Wakati waliopoteza ajira kwa kufukuzwa wakiambiwa hayo, wale wanaopoteza ajira kwa kupunguzwa (redundancy) wao wanapewa mafao yao, zingatia hawa wanaopoteza ajira kwa redundancy wana umri sawa na wale waliopoteza ajira kwa kufukuzwa kazini, na wote wapo ardhi ya Tanzania ambako hivi sasa kuna tatizo la ajira kutokana na waajiri wengi kuwa wanapunguza wafanyakazi. Huu kwa kweli ni ubaguzi na ni kanuni ya 'divide and rule'

Aya, hayo tuyaache, wakati mifuko mingine kama LAPF ikitoa fao hilo, mfuko wa PPF unazuia fao hilo. Ukienda SSRA kuhoji ili upate majibu, mamlaka hiyo ya SSRA, hawana majibu ya kueleweka, imekuwa ni vurugu tupu sawa na mechi inayochezwa refa akiwa haoni vizuri mchezo unavyoendelea, wachezaji wanakwatuana mateke yeye haoni, wachezaji wanalalamika kuhusu rafu ila refa hasikii vizuri wala kuona vizuri. Yawezekana huyu refa kalewa pombe.

Wote tukubaliane kuwa, kuna tatizo la kimawasilinao baina ya wahanga ambao ni wafanyakazi waliopoteza ajira na wale wanaotamani kuacha kazi ili wachukue mafao yao, TUCTA wenyewe ambao ndiyo wawakilishi wakuu wa wafanyakazi, SSRA ambao ndiyo mamlaka inayosimamia mifuko hii, na wabunge ambao ndiyo wanafikishiwa malalamiko haya toka kwa wahanga.

Mwisho, wakati wito wangu ni kutafuta namna ya kulijadili hili kwa marefu na mapana, niseme kuwa itakuwa kosa kubwa sana kutengeneza utaratibu kuhusu fao la kujitoa bila kuhusisha wadau wakuu ambao ni wafanyakazi. Na kwa kuwa TUCTA ni kama wapo likizo, lazima itafutwe namna ya mjadala utakaohusisha wafanyakazi wenyewe moja kwa moja. Kutengeneza utaratibu kuhusu hili la fao la kujitoa bila kuhusisha wadau wakuu ambao ni wafanyakazi, italeta tatizo. Italeta tatizo kwa sababu fedha hizo ni haki na mali ya wafanyakazi, sasa kutengeneza utaratibu bila kumhusisha mwenye mali tena mali yenyewe ni pesa, lazima italeta shida.


Solidarity Forever. For The Union Makes Us Strong!

Tamko zito fao la kujitoa

FaoLaKujitoaNipashe.JPG
 
Pesa zenu zipo kwenye uwekezaji, na sasa mifuko inaingia kwenye uwekezaji wa viwanda.

Wewe subiri faida.
 
Huu ni uonevu wa wazi kabisa mfano Nssf Arusha wankupa Mafao tu endapo utakuja na barua ya kufukuzwa kazi au mkataba wa ajira yako umekoma.kwa wale ambao wameacha kazi wenyewe wanadai kuna maagizo yametolewa kuwa wasipewe form za kudai mafao yao au uandike barua ya kujieleza kwann umeacha kazi mwenyewe.sasa hii mm naona ni unyanyasaji mkubwa sana kwa sisi tulio acha kazi mwenyewe kwa sababu mbalimbali.kama wanatoa mafao wasibague wanachama ni yupi wa kupewa na yupi wa kunyimwa,.na pia hiyo nenda njoo mwezi ujao njoo kesho na blah blah nyingi waache tufanye kazi kwa weledi kama mnvyo onekana na suti zenu mkiwa kwenye viti maridadi , cc tunapigika mjue jamani khaaa,.!tupeni chetu.
 
Hii nchi tutakuja kuigawana muda si mrefu.

Haya mambo yanakera na kuuzi. Hela yangu mwenyewe, masharti kama hela ya uchawi.
 
Kwa ujumla sisi wafanyakazi tumesalitiwa.
 
Back
Top Bottom