Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
wakuu salaam,
Kwa yeyote itakayempendeza anaweza kuichukua na kuifanyia kazi
“Suala la maendeleo ya nchi si la Rais peke yake bali yeye huonesha njia na wadau pamoja na wananchi ’kulingana na uwezo na mazingira’ husaidia kimawazo na kwa matendo ili kufikia lengo mahususi”
Katika maeneo ambayo nchi yetu bado haijaweza kuvuna rasilimali zake na kujinufaisha, ni eneo la kuvuna “mali” bahari kuu.Tanzania inalo eneo kubwa sana la bahari kuu linalojulikana kama “EEZ” (kwa mujibu wa sheria za kimataifa)ambapo nchi ina haki ya kulinda na kutumia rasilimali za eneo hilo kwa maslahi yake yanyewe. Eneo hilo lina samaki wengi, wakubwa na wanaopendwa dunia nzima maarufu zaidi wakiwa ni wale aina ya jodari (watamu hatari!).
Kwa bahati mbaya ni kwamba watanzania bado hatujaweza kuvuna vya kutosha samaki kwenye eneo hilo licha ya kwamba samaki wanazaliana kwa mabilioni na kukua hadi kufa bila kuiona ndoano ijapokuwa kwa mbali! (dah! Mali inapotea hivi hivi aisee!). Tatizo limekuwa ni mtaji wa kuwekeza kufika huko kwa kuwa inahitajika meli kubwa zenye uwezo kubwa na vifaa vya kisasa.
Kwa kuwa inaonekana rais Magufuli anatamani rasilimali za watanzania ziwanufaishe watanzania na kwa kuwa Mh.rais amekuwa akisisitiza katika kujenga viwanda Tanzania ikiwemo vya samaki na kwa kuwa soko la samaki ni la kuaminika na bei ni nzuri, na kwa kuwa kuna uhakika wa kupata samaki wa kutosha kwenye bahari kuu, na kwa kuwa samaki hao wanazaliana tu wenyewe hamna na kufuga: nashauri yafuatayo:
Mifuko ya hifadhi ya jamii iwekeze kwenye eneo la uvuvi bahari kuu kwani uwekezaji kwenye eneo hilo ni salama na wenye faida nzuri kwa kweli. Kwa kufanya hivyo, faida zifuatazo zitapatikana.
1.Kutakuwa na uhakika wa chakula (samaki) kwa watanzania, kwa kuwa mavuno ya samaki bahari kuu ni makubwa (kuna samaki wakubwa zaidi ya ng’ombe ujue!)
2. Viwanda vya kuchakata hao samaki vitajengwa na kuleta ajira kwa watanzania.
3.Watanzania watakaoajiriwa kwenye viwanda watajiunga na mfuko husika na kuchangia kama wanachama (faida itakuwa inazunguka ndani kwa ndani).
4. Serikali itakusanya kodi ya kitakachozalishwa na kuongeza mapato.
5.Mfuko utakaowekeza utatengeneza faida nzuri na ya uhakika.
6.Minofu mingine itauzwa nchi za jirani na kuingiza $’s. Hivyo kuinua uchumi wa nchi. Hizi ni faida chache tu miongoni mwa nyingi ambazo sijazitaja kufupisha mada.
Ni wito sasa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye eneo hili ambalo ni kama halijaguswa “Virgin” na lenye uhakika wa faida kwani kwa sasa mifuko yote inawekeza kwenye majengo, na miaka kadhaa ijayo upo uwezekano wa mifuko hiyoo kujikuta ikiwa imejenga majengo mengi kuliko wapangaji na kujikuta wakipata hasara kwa kukosa wapangaji wa kutosha.Ni vema kuiona fursa hii na kwa pamoja tukajenga uchumi wan chi yetu.
Asanteni.