VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
CCM inashangaza. Sasa inataka midahalo ya wagombea wa Urais kutoka vyama vyote. Kabla ya mwaka huu,CCM imekuwa ikipiga vita na kukataza midahalo inayowahusisha wagombea wetu au hata makada tu. Ilikatazwa kiofisi na Luteni Mstaafu Yusuph Makamba,alipokuwa Katibu Mkuu wa CCM.
CCM imekuwa ikikimbia na kuepuka midahalo isipokuwa vipindi vya redioni na luningani vinavyoandaliwa kimkakati. Mwaka huu,CCM inajipambanua kama inayotaka midahalo. Yote haya ni kwasababu mgombea wa CHADEMA/UKAWA ni Edward Lowassa.
CCM haitaki midahalo kwasababu Dr. Magufuli anajiweza sana. Au anajua kujenga hoja. Au anajua mambo ya kisiasa,kiuchumi na kijamii na hata kimataifa. Ila ni kwakuwa upande ule kuna Lowassa. Inaaminiwa kuwa Lowassa ni mgonjwa. Inasadikiwa kuwa Lowassa hawezi kuzungumza kwa muda mrefu. Lengo ni kumuanika. Kumuaibisha.
Hofu yangu ni kuwa Lowassa aweza kuwa imara na mwenye uwezo mkubwa wa kuongea kwa muda mrefu. CCM itajitumbukiza kwenye aibu ya karne kwakuwa Dr. Magufuli hajui chochote zaidi ya idadi ya mifugo na samaki pamoja na barabara na madaraja.
Ni hadaa na mzaha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam