Michezo na siasa Tanzania: TFF mpo kweli?

Michezo na siasa Tanzania: TFF mpo kweli?

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2007
Posts
396
Reaction score
68
Taarifa zilizotufikia kutoka kwa wadau ni kuwa mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo ameagiza TFF ifanye uchaguzi kwa kutumia katiba ya 2006. Tunachokiona; siasa ikiingilia michezo FIFA itatufungia. Maana yake ni kwamba timu zetu hazitashiriki mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu. Tusubiri tuone mwisho wake.
 
Mpira wa tanzania hushangaza sana!mpira huchezwa mezani,hakuna kanuni zinazofuata!wewe subiri huyo huyo waziri atakuja sema AMENUKULIWA VIBAYA
 
Hata mimi nimemsikia waziri fenela mkangala kuwa wanataka itumike katiba ya 2006. Hivi hawajui kuwa fifa walishatuma ujumbe kwa ajili ya kushughulikia uchaguzi wa tff? Ninahisi nchi ikiendelea na msimamo huo inaweza kufungiwa kwa sababu ya serikali kuingilia soka kama ilivyowahi kutokea kwa ethiopia na nchi nyingine hivi karibuni kabal ya serikali zao kujirudi.
 
Welldone Wambura. kazi yako ya ulinzi shirikishi dhidi ya TFF, imejibu. Fifa wakitufungia naona itakuwa poa tu, ili tupate nafasi ya kuziandaa vyema timu zetu za taifa na vilabu.
 
mpira wa tanzania hushangaza sana!mpira huchezwa mezani,hakuna kanuni zinazofuata!wewe subiri huyo huyo waziri atakuja sema amenukuliwa vibaya

uamuzi wa waziri una madhara mengi. Moja ni kwamba masindano ya ligu kuu ya 2011/2012 yaliendeshwa kinyume na katiba na hivyo ni batili. Hapa ina maana kuwa ushindi wa simba na azam na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa ni batili. Pili, ligi inayoendelea sasa 2012/13 ni batili na kwamba mshindi atakaye tangazwa ni batili. Tatu, upo wasiwasi mkubwa sana kuwa waziri kwa maslahi binafsi ameamua kwa makusudi kujiingiza kwenye suala hili bila kujali athari zake. Wote tunafahamu kuwa mhe. Makala alikuwa katibu mwenezi wa simba na kwa msingi huo asingependa kuona yanga inasonga mbele hasa baada ya simba kuwa inafanya vibaya kwenye ligi. Tunafahamu pia uhusiano wa waziri na familia ya malinzi na nini anatarajia kutoka kwao. Tungoje tuone tff watasema nini.
 
Taarifa zilizotufikia kutoka kwa wadau ni kuwa mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo ameagiza TFF ifanye uchaguzi kwa kutumia katiba ya 2006. Tunachokiona; siasa ikiingilia michezo FIFA itatufungia. Maana yake ni kwamba timu zetu hazitashiriki mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu. Tusubiri tuone mwisho wake.

Hivi tukifungiwa na FIFA tunapata hasara gani economically, politically. I can understand on world socialisation! najaribu tukifungiwa kupata subsidy ya ARV, ALu (malaria drug), various subsidized children's vaccines!!!
 
Nadhani ni wakati muafaka tufungiwe ili tujipange upya
 
uamuzi wa waziri una madhara mengi. Moja ni kwamba masindano ya ligu kuu ya 2011/2012 yaliendeshwa kinyume na katiba na hivyo ni batili. Hapa ina maana kuwa ushindi wa simba na azam na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa ni batili. Pili, ligi inayoendelea sasa 2012/13 ni batili na kwamba mshindi atakaye tangazwa ni batili. Tatu, upo wasiwasi mkubwa sana kuwa waziri kwa maslahi binafsi ameamua kwa makusudi kujiingiza kwenye suala hili bila kujali athari zake. Wote tunafahamu kuwa mhe. Makala alikuwa katibu mwenezi wa simba na kwa msingi huo asingependa kuona yanga inasonga mbele hasa baada ya simba kuwa inafanya vibaya kwenye ligi. Tunafahamu pia uhusiano wa waziri na familia ya malinzi na nini anatarajia kutoka kwao. Tungoje tuone tff watasema nini.

Umesema waziri ni shabiki wa simba na kwamba ana uhusiano na familia ya Malinzi, je wewe una mahusiano na Tenga?
Madhara uliyotaja yanaweza kutukuta lakini kumbuka si busara kukiuka kanuni na taratibu. Toa hoja kama vigezo alivyovitaja waziri si sahihi.
 
Waziri kachemka halafu nilikua namsikiliza jana anaongea hadi povu linamtoka kwa jazba..
 
Back
Top Bottom