Asghal na Temba X-Mass
Saturday, 25 December 2010 11:25
Zaina Malongo
MSANII mchanga wa muziki wa kizazi kipya Ally Goloto a.k.a Asghaly mwenye maskani yake Kurasini Jijini Dar es Salaam amevunja mkataba na kundi la BBM Grew na kuamua kutoka mwenyewe.
Akizungumza na starehe amesema kutoka mwenyewe baada ya kundi hilo kutokana na kundi lkutokuwa na msimamo utendaji kisanii .
"Nimeamua kutoka mwenyewe na singo yangu moja nitakayoitambulisha kwa washabiki kwa jina la ‘Mapenzi sio Pesa' ambapo nimeshirikisha Temba wa kundi la wanaume famili kutokana na kumkubali katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya"amesema Goloto
Goloto amesema amekaa kimya kwa miaka mitatu kutokana na kukoza mdhamini wa kumtoa kimuziki ikiwa muziki kwa upande wake upo katika damu.
Amesema bado ajafanikiwa kivile hivyo ameweka milango wazi kwa msamaria ambae ataweza kumtoa kimuziki kwani malengo yake kimuziki ni makubwa kwa nchi ya Tanzani hasa katika kuitangaza.