Ferguson aweka rekodi ya kufundisha muda mrefu zaidi United
Monday, 20 December 2010 20:11
LONDON, England
SIR Alex Ferguson anakuwa kocha wa kwanza aliyeitumikia Manchester United pamoja na kutofanyika kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Chelsea kutokana na kuaguka kwa barafu nyingi.
Kwa kukaa siku 8,811, Ferguson mwenye miaka 68 ameipiku rekodi iliyowekwa na Mscotland mwenzake Matt Busby aliyekaa Old Trafford kwa siku 8,809.
"Ameweka historia katika soka, kocha bora ni Sir Alex," alisema kocha wa England, Fabio Capello, (64) ambaye amewahi kuzifundisha Real Madrid na AC Milan. "Kwa muda wote aliokuwa hapa ameweza kuiongoza vema timu yake na kufanya mabadiliko makubwa. Amebadilisha kabisa timu, amebadilisha wachezaji, amekuwa ni mtu muhimu, muhimu sana kwa klabu yake."
Ferguson ambaye ametwaa mataji 26, tangu alipochukua timu hiyo kutoka kwa Ron Atkinson mwezi Novemba 1986, mataji aliyochukua ni pamoja na Ligi Kuu mara 11 na Ligi ya Mabingwa mara mbili.
"Ni mafanikio makubwa," alisema kocha msaidizi wa United, Mike Phelan, ambaye pia alikuwa mchezaji wakati wa Ferguson. "Siri ya mafanikio yake kujiamini, anafanya kazi kwa mipango na kufutwa kanuni ni kitu alichozaliwa nacho, kinatokana na asili ya familia yake."
Ferguson, ambaye alifuta mjadara wa kuhusu uwezekano wake wa kustaafu baada ya kutangaza kuendelea na kazi yake, alipewa tuzo ya heshima ya 'knighthood' na Malkia Elizabeth II mwaka 1999 baada ya kuiongoza United kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA mwaka huo.
Pia amekuwa ni kocha aliyepeta mafanikio zaidi katika soka ya Uingereza, Ferguson alivunja mapema rekodi ya Busby ambaye aliichukua United kwenye kipindi kigumu kufutia ajari ya ndege ya mwaka 1958 Munich iliyochukua maisha ya wachezaji wa nane.
Busby aliiongiza klabu hiyo kutwaa taji la kwanza la Ulaya mwaka1968, pamoja na kuipa mataji matano ya Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza kuanzia kati ya mwaka 1945 hadi 1969. Alirudi tena kuifundisha timu hiyo kuanzia mwaka 1970 hadi 1971 baada ya hapo alipaki kuwa mshauri wa ufundi hadi kifo kilipomkuta mwaka 1994, akiwa na miaka 84.