Real Madrid, Barcelona zaongoza kwa utajiri
Thursday, 10 February 2011 20:56
LONDON, England
KLABU za Real Madrid na Barcelona ziko kwenye klabu bora 20 kwa kuingiza dola 5.5 billion kwa mara ya kwanza.
Taarifa ya mapitio ya ukaguzi wa fedha uliofanyiwa na kampuni ya Deloitte unaonyesha kuwa, Madrid wameingiza euro 438.6 million (dola539.1 million) katika mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 na klabu hiyo kendelea kuongoza kwa kuingiz amapto zaidi.
Barcelona, iliyoifunga Madrid na kutwaa ubingwa wa klabu bingwa ya dunia 2009, imechukua nafasi ya pili, lakini kwa kuingiza mapato chini ya silimia 10 kiasi cha euro 398.1 milioni sawa na dola 489.3 milioni..
Fedha zinazopatikana ni kutokana na mapato ya mechi, kuuza bidhaa za klabu na mapato mbalimbali.
Wengine walioko kwenye sita bora kwa kuingiza mapato mengi ni pamoja na Manchester United inayoshika nafasi ya tatu, ikifuatiwa na Bayern Munich, Arsenal na Chelsea.
Kati ya klabu kuu 20 zinazotesa ni pamoja na Manchester City, ikishika nafasi ya tisa kutoka ya 11 na pato lake ni asilimia 44 ya mapato yote ambayo ni pauni125 milioni (dola187.8 milioni).
Liverpool imeshuka nafasi moja hadi ya nane baada ya kumaliza ya saba na hiyo ni kutokana an kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Klabu zote 20 zimeongeza pato lake mwaka 2009-10 licha ya kuwepo kwa mdororo wa kiuchumi ulioikumba dunia mwaka jana," Dan Jones wa Kundi la Makampuni ya Biashara ya Deloitte alisema.
"Klabu kubwa zimejipanga zenyewe kupata fedha licha ya kukumbwa na sakata la kudorora kwa uchumi, uwezo wa kutangaza mechi, na kuongeza vivutio kwa wawekezajki ndani ya klabu."