Tegete, Gumbo watemwa Stars, Mgosi, Banka warudishwa
Imeandikwa na Evance Ngingo; Tarehe: 4th February 2011 @ 23:55
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Jan Poulsen ametangaza kikosi chake kipya huku akiwaacha Jerry Tegete wa Yanga, Rashid Gumbo wa Simba na nyota wote wanaocheza soka nje ya Tanzania.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 22 amewaita kwa mara ya kwanza beki Chacha Marwa wa Yanga, Julius Mrope wa Mtibwa Sugar, Ramadhan Chombo wa Azam, huku akiwarudisha beki Juma Jabu na Haruna Shamte wote wa Simba.
Wengine ambao amewarudisha tena kwenye kikosi hicho ni Mussa Mgosi na Mohammed Banka wa Simba pamoja na John Bocco wa Azam.
Kiungo Godfrey Bonny wa Yanga ambaye kwa muda mrefu hayupo kwenye kikosi cha Taifa Stars naye amekumbukwa.
Akizungumza jana, Poulsen alisema kikosi hicho ni kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na Palestina utakaofanyika Februari 9, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia sababu za kumwacha mchezaji Ali Ahmed Shibori, Paulsen alisema kuwa mchezaji huyo anatakiwa kujiendeleza zaidi hasa kwa kujifunza kasi na kuongeza uwezo wa kucheza.
Wachezaji wanaocheza nje ya nchi wote amewaacha ambao ni Athumani Machupa (Sweden), Said Maulid (Angola), Idriss Rajabu (Kenya), Henry Joseph (Sweden) na Nizar Khalfan (Canada).
Ruta: asante ripoti kamili juu ya kikosi cha timu ya Taifa:
Niko pembezoni mwa nchini kiasi kwamba magazeti huwa tunayapata baada ya siku moja.
Kumbe na Kelvini Yondani naye kaachwa!!!!!
[/QUOTE