Mwamuzi aondolewa 9Bora Tanga
Wednesday, 02 February 2011 20:36
Calvin Kiwia
IKIWA leo ni siku ya mapumziko Fainali za ligi Daraja la Kwanza zinazoendelea kutimua vumbi lake uwanja wa Mkwakwani Tanga, Kamati inayosimamia ligi hiyo, imemwondoa mwamuzi msaidizi, Richard Kayenza kutokana na kupindisha sheria 17 za soka.
"Sisi kazi yetu kuu ni kuhakikisha masuala yote yanakwenda vema kwenye kituo hiki kwa wachezaji na waamuzi wanachezesha kwa kufuata sheria?," alisema Kiondo.
"Tumemwondoa kwenye orodha zetu mwamuzi wa pembeni, Richard Kayenze kutoka Kigoma aliyechezesha mchezo kati ya Coastal Union na Villa Squad, kwa kosa la kupindisha taratibu na sheria 17 za soka kwenye mchezo huo uliomalizika kwa wenyeji kushinda bao 1-0 ," aliongeza.
Alisema kuwa kuondolewa kwa mwamuzi huyo, itakuwa fundisho kwa waamuzi wengine wenye lengo tofauti na sheria 17 za soka.
Hata hivyo, alisifu ushindani uliopo kati ya timu shiriki za ligi hiyo inayoshiorikisha timu tisa. Timu nne ndizo zitakazopanda Ligi Kuu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa kuwakutanisha maafande wa Oljoro JKT dhidi ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kutokana na timu hizo kutandaza kabumbu la kueleweka.