Aliyeshindwa ZFA amdai Ferej Sh100mil Monday, 31 January 2011 20:55
Salma Said, Zanzibar
RAIS wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka Zanzibar, ZFA, Ali Ferej Tamim ameingia katika wakati mgumu baada ya waliokuwa wagombea nafasi ya urais na makamu wa ZFA kumpa wiki moja na awalipe fidia ya sh100mil kwa madai ya kuwakashifu .
Hatua hiyo inakuja wakati Fereji na wenzake kurudishwa madarakani kwa muda wa miezi mitatu ili warekebishe katiba ya chama hicho na kuandaa uchaguzi mkuu mwingine baada ya ule wa awali kubatilishwa
Walalamikaji ni pamoja na aliyekuwa mgombea urais, Suleiman Mahmoud Jabir na makamu wake, Aman Ibrahim Makungu ambao walidai Ferej aliwakashifu mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu uliofanyika Desemba 31 mwaka jana.
Barua ya kampuni ya mawakili AJM Solicitors of Advocate Chamber yenye kumbukumbu namba KK.NO.AJM/MJD/019/2011 ya Januari 20 mwaka huu na kusainiwa na wakili Rajab Abdalla Rajab na kutumwa kwa Ferej, ilidai kashfa hizo zilitolewa wakati kiongozi huyo akitoa hutuba ya mkutano mkuu.
Amedai kauli za Ferej mbele ya wajumbe zimepelekea wateja wake ziwashushie hadhi mbele ya jamii na kuwajengea dhana kuwa ni watu wasiofaa katika jamii kwa tuhuma nzito ambazo hakuwa na uhakika nazo.
Katika tuhuma zilizoelekezwa kwa Makungu imedaiwa Ferej aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa ni mtoa rushwa na mara zote amekuwa akiwahonga viongozi wa ZFA ili timu yake iweze kushinda na hivyo ni mchangiaji mkuwa wa kuuwa soka la Zanzibar
ìTuhuma hizo nzito zisizokuwa na uthibitisho mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu na waalikwa zimemuumiza mteja wangu na kumshushia hadhi yake mbele ya jamii na hivyo kusababaisha athari kubwa,î ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
ìWateja wangu ni watu maarufu san a na wanaheshima kubwa katika jamii kupitia vyombo vya Habari nakutaka uwaombe radhi wateja wangu dhidi ya tuhuma ulizozitoa zilizokosa chembe za ukweli îInasomeka barua hiyo ya kurasa mbili
Madai hayo kwa Rais huyo yamekuja zikiwa zimepita siku chache tangu iliyokuwa kamati ya uchaguzi wa chama hicho ibatilishe matokeo ya uchaguzi kutokana na kujitokeza mapungufu mengi ya Fereji kushindwa kuthibitsha elimu ya kidato cha nne
Hata hivyo, habari nyengine zinadai kesi inayohusu wadau wa soka iliyowasiliswa mahaka kuu dhidi ya Ferej na wenziwe huenda ikaanza kutajwa wiki ijayo baada ya kupangiwa Jaji Abraham Mwampashe aisikilize
Wamaolalamikiwa ni Ferej , Makamo wa Rais Haji Ameir ,Mrajis wa vyama vya michezo Mustafa Omar ,Katibu mkuu wa ZFA, Mzee Zam Ali na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Sherry Khamis
Madai makuu ya shauri hilo ni kwamba kwa nyadhifa zao walishindwa kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa ZFA huku wakijuwa umejaa mapumgufu mengi ya kikatiba na kwamba Rais na Makamo wake hawana uhalali wa kuongoza chama hicho kwa vile muda wao ulimalizika tangu Septemba 30 mwaka jana.